Mr Bones

Mr Bones ni filamu ya vichekesho iliyoigizwa mnamo mwaka 2001 nchini Afrika Kusini.

Kichwa cha filamu kinabeba jina la mhusika mkuu ambaye kwa jina halisi anaitwa Leon Schuster. Leon Schuster pia ndiye aliyeandika kisa cha filamu hiyo na kushirikiana katika kuandika jinsi itakavyo igizwa. Filamu hii inalezea juu ya tamaduni za kiafrika dhidi ya tamaa na uchoyo katika taifa la Afrika kusini pia ikizungumzia tamaduni za kiafrika dhidi ya mitindo ya ubaguzi.

Filamu hii iliweza kukusanya pesa takribani R33 milioni, na kuifanya kuwa filamu ambayo imekusanya mapato mengi huko nchini Afrika kusini kwa wakati wote mpaka pale ilipokuja kupitwa na muendelezo wake wa filamu ya Mr Bones 2: Back from the Past ambayoilikusanya mapato ya pesa takribani R35 milioni. Filamu hii ilizidiwa na Titanic katika historia ya mauzo ya filamu ya nchini Afrika Kusini.

Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mr Bones kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.