Mto Amanzimtoti (hufahamika pia kama Manzimtoti) ni mto mfupi katika jimbo la KwaZulu-Natal, Afrika Kusini.
Una asili kaskazini mashariki mwa misioni ya Adamu na humwaga maji yake kwenye mji wa Amanzimtoti, Afrika Kusini na huishia Bahari ya Hindi.
Mfalme Shaka Zulu anasemekana alilipa jina mto huu baada ya kunywa maji na kusema kwa mshangao kwa kizulu "Kanti amanzi mtoti" ("maji matamu").
Hivi karibuni kumekuwa na mapendekezo rasmi ya kubalisha jina la mto kuwa Manzamtoti ili liwe na maana na uhalisia katika matamshi na maandishi ya Kizulu. Ingawa wenyeji wa Amanzimtoti bado wanapendelea kutumia mto kama Amanzimtoti, mto Mazimtoti au mto Toti.
Mbinu mbadala ya hivi karibuni na isiyo maarufu, mapendekezo ya jina la asili la mto liko kwenye maneno ya kizulu Udoti ikimaanisha uchafu ambalo linakaribiana kufanana na 'toti', na jina linamaanisha maji machafu.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Amanzimtoti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |