Mto Apies

Mtao Apies unapopita ndani ya Bustani ya wanyama mjini Pretoria

Mto Apies ni mto unaopita katika mji wa Pretoria, Afrika Kusini. Chanzo chake ni umbali mdogo upande wa chini wa mji, unatiririka ndani yake hadi kuishia katika mto Pienaars.[1] Mto huu unajulikana kama Apiesrivier kwa lugha ya Kiafrikaans "Apies" ambayo inamaanisha nyani mdogo. Hii ni kwa mujibu wa kupatikana kwa vima aina ya ngedere.

Watu wa kwanza waliojenga makazi hapa walikuwa wasemaji wa Kingoni asilia waliojulikana baadaye kwa jina la Wandebele, walikuta Wakhoikhoi wahamiaji wasiokuwa na vijiji vya kudumu. Wandebele waliita mto huu "Tshwane'" na kuna majadiliano kuhusu maana asilia ya jina hilo. Wengine husema Wandebele walitumia jina la abaTshwa kwa hao Wakhoikhoi, hivyo jina lilirejelea watu waliowakuta katika sehemu hizi. Wengine wanasema kwamba Tshwane ilikuwa jina la chifu wa Wandebee aliyezikwa kando la mto. Kwa jumla mto bado hutajwa zaidi kwa jina la Kiafrikaans.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Gauteng State of the Environment Report 2004" (PDF). Gauteng Provincial Government. uk. 4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-01-21. Iliwekwa mnamo 2009-01-27. {{cite web}}: More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Apies kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.