Muda

Saa ya kwazi.

Muda ni kipindi ambacho mtu aidha alifanya, anafanya au anatarajia kufanya jambo fulani. Katika maisha tumepitia vitu mbalimbali, baadhi tunaweza tukavikumbuka na vingine hatuvikumbuki, na katika maisha kadri muda unavyokwenda ndivyo vitu vinazidi kugunduliwa kutokana na ongezeko la sayansi.

Katika maisha ya kila siku mwanadamu hutegemea sana muda ili kufanikisha malengo yake.

Matumizi ya muda

[hariri | hariri chanzo]

Muda hutumika na watu mbalimbali kwa mambo mbalimbali kama itakavyoelezwa hapa chini:

  1. mwanafunzi hutumia muda wake hasa kwa ajili ya kujisomea.
  2. mfanyakazi hutumia muda wake hasa kwa ajili ya kujiendeleza kimaisha.

Endapo watautumia muda huo vibaya, hakika hawataweza kufikia malengo waliyojiwekea.

Hata hivyo ni muhimu kuwa na uwiano mzuri katika matumizi ya muda, kwa mfano, kwa sala na kazi.