Nada Topčagić; amezaliwa Modriča, Yugoslavia, 3 Julai 1953) ni mwimbaji toka Bosnia na Herzegovina.
Kazi yake ilianza mwaka 1975, kwa kutoa wimbo wake wa kwanza, "Na Drini ćuprija" (Daraja juu ya “Drina”), uliyoandikwa na Obren Pjevović. Alikuwa maarufu sana kipindi cha miaka ya 1980 ingawa bado anasikika mpaka leo. Mwezi mmoja baada ya kuanguka kwa Vukovar kwenye vita vya uhuru vya Kroatia, kwenye majira ya baridi ya 1991-92, yeye, Era Ojdanić na Mira Kosovka waliimba katika tamasha kwa ajili ya wanajeshi wa Kiserbia kwenye mji uliotekwa.[1][2].[3] Kulingana na yeye, alilazimishwa na kikosi cha jeshi kuimba katika tamasha. Mwaka 2021, mchezaji wakiswedishi Zlatan Ibrahimović alitumia kipande cha wimbo wake "Jutro je" (Ni Asubuhi) katika Tamasha la Muziki la Sanremo. Kipande cha muziki baadae kilipata umaarufu mkubwa.
Topčagić alitoka Bosnia na Herzegovina na kwenda Belgrade muda fulani kabla ya kutoa wimbo wake wa kwanza (1975). Nada anaishi na kufanya kazi. Ameolewa na Zlatko Đorđević, pamoja naye ana mtoto wa kiume, Miroslav (alizaliwa 1984).[4]
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
![]() |
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nada Topčagić kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |