Nadhiri ya nne ni nadhiri ambayo inadaiwa na watawa wa mashirika kadhaa zaidi ya zile tatu za msingi kwa wote zinazohusu mashauri ya Kiinjili ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu.
Ni nadhiri inayotokeza kwa namna ya pekee tabia na karama ya shirika, kama vile kujitoa hadi kufa kwa ajili ya Wakristo walio katika hatari ya kupoteza imani (Wamersedari), kushika matendo ya toba ya kwaresima mwaka mzima (Waminimi), kumtii Papa katika kutumwa naye (Wajesuiti), kutumikia walio fukara zaidi kati ya mafukara (Wamisionari wa Upendo wa Mama Teresa wa Kolkata).
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nadhiri ya nne kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |