Nahid Toubia (kwa Kiarabu: ناهد طوبيا [1]; alizaliwa Khartoum, Sudan[2], mnamo mwaka 1951[3]) ni raia wa Sudan anayefanya kazi za upasuaji na mwanaharakati wa haki za afya za wanawake akiwa ni mbobevu katika utafiti katika ukeketaji wa wanawake.[2].
Pia ni mwanzilishi na mkurugenzi wa RAINBO.[2].
Nahid pia ni profesa wa ushirika katika Chuo Kikuu cha Columbia kitivo cha Afya ya Umma. ni mwanakamati wa kisayansi na ushauri kwa Shirika la Afya Duniani, UNICEF, na UNDP. Yeye pia ni makamu ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mradi wa Haki za Wanawake wa Human Rights Watch[4].
Toubia alianza kusoma shule ya msingi na ya kati katika shule ya kanisa la ndani.[5] Hata hivyo kwa sababu ya ukosefu wa elimu ya binafsi nchini Sudan alichukua ruhusa ya usajili kumruhusu kuingia shule ya sekondari ya Khartoum ya wasichana. Kisha akapata elimu ya Chuo Kikuu cha Kharmoum kwa masomo ya maandalizi ya matibabu kwa mwaka mmoja. Kisha akafuata kazi kama daktari, huku akisoma shule ya matibabu nchini Misri. Mnamo mwaka 1981 alikamilisha mafunzo yake ya upasuaji nchini Uingereza, kupata (MpHIL) na Shahada ya uzamivu ya Afya ya Umma na Sera kutoka Shule ya London ya Usafi na Dawa ya Tropical
Toubia ni mwandishi wa vitabu kadhaa ikiwa ni pamoja kitabu cha wanawake wa ulimwengu wa Kiarabu,
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nahid Toubia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |