'
Nancy Sumari | |
---|---|
Nancy akiwa na Mama Salma Kikwete. | |
Amezaliwa | 7 Agosti 1986 Arusha |
Nchi | Tanzania |
Kazi yake | Mwanamitindo |
Taji | Miss Tanzania 2005 |
Ndugu | Nakaaya |
Nancy Abraham Sumari (alizaliwa 7 Agosti 1986) alikuwa mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2005 na Mrembo wa Dunia wa Afrika kwa mwaka 2005.
Nancy Sumari alizaliwa mkoani Arusha Tanzania, akiwa mtoto wa tatu katika familia ya Abraham Simango Sumari, akiwa na dada yake Glory aliyekuwa anampa hamasa na ushauri zaidi juu ya masuala ya urembo. Ndugu zake wengine katika ukoo wao ni Devis, Patra, Tumo na Nakaaya Sumari.
Alipata elimu yake ya msingi mjini Nairobi, Kenya katika shule ya msingi ya Blue Bells. Baadaye kuingia elimu ya Sekondari ya wanawake ya Maasai ya huko huko Nairobi ’NBO’ na kuhitimu mwaka 2004 na baadae kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam akisomea masuala ya utawala wa biashara.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nancy Sumari kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |