Nyoka mdomo-kulabu | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nyoka mdomo-kulabu (Scaphiophis albopunctatus)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 2:
|
Nyoka mdomo-kulabu ni nyoka wa jenasi Scaphiophis katika familia Colubridae. Wamepewa jina hili kwa sababu mdomo wa juu una umbo wa kulabu kama domo la kipanga.
Nyoka hawa ni warefu kiasi, m 1.6 kwa kipeo lakini m 0.9-1.3 kwa kawaida. Rangi ya mgongo ni kijivu au kahawia, ile ya mbavu ni kijivu, kahawia, kahawianyekundu au machungwa na ile ya tumbo machungwa, pinki au maziwa. Ndani ya mdomo ni nyeusi.
Nyoka mdomo-kulabu huishi katika vishimo au huchimba katika udongo tifutifu. Hula wagugunaji ambao wanakamata katika vishimo. Labda hula mayai pia.
Nyoka hawa hawana sumu na huyaua mawindo kwa kuwabamiza dhidi ya ukuta wa kishimo. Wakitishwa huachama mdomo ili kuonyesha rangi ya nyeusi. Kisha huinua kichwa juu na wanaweza kushambulia pia, lakini hawang'ati.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyoka mdomo-kulabu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |