Ofisa (pia: afisa, kutoka Kiingereza: officer) ni mtu mwenye cheo katika ofisi au katika mfumo wa shirika fulani. Neno latumiwa hasa kwa wanajeshi wa vyeo vyenye mamlaka juu ya wanajeshi wa kawaida.
Katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyeo vya maofisa vimepokewa kutoka jeshi la kikoloni vikifuata mfumo wa jeshi la Uingereza.
Maofisa hutofautishwa baina ya wenye kamisheni (ambavyo ni vyeo vya juu zaidi) na maafisa wa ngazi za chini.
(Cheo cha Kitanzania - (Cheo cha Kiingereza)
Afisa Mteule Daraja la Kwanza (Warrant Officer Class 1) |
Afisa Mteule Daraja la Pili (Warrant Officer Class 2) |
Sajinitaji (Staff Sergeant) |
Sajini Sergeant) |
Koplo (Corporal) |
Koplo Usu (Lance Corporal) |
(Cheo cha Kitanzania - (Cheo cha Kiingereza)
Jenerali (General) |
Luteni Jenerali (Lieutenant General) |
Meja Jenerali (Major General) |
Brigedia Jenerali (Brigadier General) |
Kanali (Colonel) |
Luteni Kanali (Lieutenant Colonel) |
Meja (Major) |
Kapteni (Captain) |
Luteni (Lieutenant) |
Luteni usu (Second lieutenant) |
Ofisa Mwanafunzi Officer cadate) |