Paricalcitol

Paricalcitol
Jina la (IUPAC)
(1R,3R,7E,17β)-17-[(1R,2E,4S)-5-hydroxy-1,4,5-trimethylhex-2-en-1-yl]-9,10-secoestra-5,7-diene-1,3-diol
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Zemplar
AHFS/Drugs.com Monograph
MedlinePlus a682335
Kategoria ya ujauzito C(AU) C(US)
Hali ya kisheria Prescription Only (S4) (AU) -only (CA) POM (UK) -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Kwa mdomo, kwa mishipa
Data ya utendakazi
Uingiaji katika mzunguko wa mwili 72%[1]
Kufunga kwa protini 99.8%[1]
Kimetaboliki Katika ini[1]
Nusu uhai Masaa 14-20 [1]
Utoaji wa uchafu Kinyesi (74%), mkojo (16%)[1]
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Visawe 19-nor-1,25-(OH)2-vitamini D2
Data ya kikemikali
Fomyula C27H44O3 
  • InChI=1S/C27H44O3/c1-18(8-9-19(2)26(3,4)30)24-12-13-25-21(7-6-14-27(24,25)5)11-10-20-15-22(28)17-23(29)16-20/h8-11,18-19,22-25,28-30H,6-7,12-17H2,1-5H3/b9-8+,21-11+/t18-,19+,22-,23-,24-,25+,27-/m1/s1 YesY
    Key:BPKAHTKRCLCHEA-UBFJEZKGSA-N YesY
 N(hii ni nini?)  (thibitisha)

Paricalcitol, inayouzwa kwa jina la biashara la Zemplar, ni dawa inayotumika kuzuia na kutibu shida ya tezi parathyroidi (hyperparathyroidism) kutokana na ugonjwa sugu wa figo.[2] Inachukuliwa kwa mdomo.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhara, athari za mzio, kichefuchefu, maumivu ya kichwa na shida ya kulala.[3] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha sumu ya juu ya kalsiamu na alumini.[3] Kuna wasiwasi juu ya matumizi yake katika ujauzito.[2] Ni aina ya calcitriol, aina hai ya vitamini D.[3]

Paricalcitol ilipewa na hati miliki katika mwaka wa 1989 na kuidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu mwaka wa 1998.[4] Dawa hii inapatikana kama dawa ya kawaida.[3] Nchini Uingereza, dozi 28 za mikrogramu 1 ziligharimu Huduma ya Kitaifa ya Afya (NHS) takriban £70 kufikia mwaka wa 2021.[2] Kiasi hiki nchini Marekani ni takriban dola 100 za Marekani.[5]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Zemplar (paricalcitol) dosing, indications, interactions, adverse effects, and more". Medscape Reference. WebMD. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Februari 2014. Iliwekwa mnamo 26 Januari 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1137. ISBN 978-0857114105.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 "Paricalcitol Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Februari 2021. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Fischer, Jnos; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-based Drug Discovery (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 452. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-22. Iliwekwa mnamo 2021-03-18.
  5. "Paricalcitol Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)