Peter Kenneth

Peter Kenneth
Peter kenneth
Peter kenneth
Waziri msaidizi Wizara ya Mipango,
Maendeleo na Vision 2030
Jimbo la uchaguzi Gatanga
Tarehe ya kuzaliwa 27 Novemba 1965
Mahali pa kuzaliwa Kirwara
Chama Kenya National Congress
Alingia ofisini 2002
Dini Mkristo
Elimu yake Chuo Kikuu cha Nairobi,
Digrii anazoshika Sheria
Kazi Mwanabenki
Mwanasiasa[1]
Tovuti yake Tovuti rasmi


Peter Kenneth (alizaliwa 27 Novemba 1965) ni mwanasiasa wa Kenya. Yeye anatoka katika familia mashuhuri ijulikanayo kama Muhuni (kwa Kikikuyu) ya eneo la Kirwara katika eneo bunge la Gatanga huko kaunti ya Murang'a[2]

Maisha ya awali na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Peter Kenneth alihudhuria Shule ya Msingi ya Uhuru (CPE) huko Bahati na baadaye akajiunga na shule ya upili ya Starehe Boys kwa masomo yake ya ngazi ya 'O' al maruf O levels. Yeye ni mmiliki wa shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, na Mtendaji wa Taasisi ya Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Usimamizi cha Lausanne, Uswisi. Yeye pia alisomea uhasibu na uana benki pamoja na masomo ya bima.Baada ya kufuzu kama mwanabenki alifanya kazi katika taasisi kadhaa.[3]

Nationwide Finance company

[hariri | hariri chanzo]

Alianza kufanya kazi katika kampuni ya Nationwide Finance katika mnamo 1985 hadi 1986.

Prudential Finance and Bank

[hariri | hariri chanzo]

Hapo baadaye, alifanya kazi katika benki ya prudential kwa takriban miaka kumi na moja kuanza 1986 hadi 1997. Wakati wa kukaa kwake hapa, alipanda vyeo hadi akafikia kuwa meneja.

Kenya Football Federation

[hariri | hariri chanzo]

Alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya mnamo 1996 nafasi ambayo alihudumia mpaka mwaka wa 2000.[4]

Kenya Reinsurance Company

[hariri | hariri chanzo]

1997, alijiunga na kampuni ya Kenya Reinsurance na akafanya kazi hadi 2002.

Africa Reinsurance Corporation

[hariri | hariri chanzo]

Mkurugenzi wa biashara kutoka 1998 hadi 2001

Zep Reinsurance Company

[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa mwenyekiti wa kampuni ya Zep rensurance tangu 1998 hadi 2009.

Maisha ya kisiasa

[hariri | hariri chanzo]

Kenneth alichaguliwa mara ya kwanza bungeni kama mwakilishi wa eneo bunge la Gatanga mnamo Desemba mwaka wa 2002 kwa tiketi ya National Rainbow Coalition. Amedumu katika wadhifa huu hadi sasa.[5]

Amehudumu katika wizara kadhaa kama waziri msaidizi zikiwemo ni pamoja na; Wizara ya maendeleo ya ushirika na masoko kati ya Novemba 2003 hadi 2005, wizara ya fedha kati ya Desemba 2005 na 2007 na wizara ya nchi ya mipango, maendeleo ya Taifa na Vision 2030 ambapo amehudumu tangia mwaka wa 2008 hadi sasa.

2007-2012

[hariri | hariri chanzo]

Chini ya uongozi wa Peter Kenneth, eneo mbunge la Gatanga lilichaguliwa kama lililotumia pesa za Constituency Development Fund (CDF) kwa njia iliyo bora zaidi katika mwaka wa fedha wa 2011/2012.[6][7]

Jitihada za kuwa Rais

[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa wa kwanza kati ya wagombeaji wote wa urais katika uchaguzi mkuu ujao wa Kenya unaotarajiwa kufanyika mwaka wa 2013.[8]Wakati wa uzinduzi wa kampeni zake hapo 2011, alisema angeweza kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Kenya National Congress. Aliahidi kuwa atahakikisha kwamba serikali yake itaangazia maswala kumi na tatu muhimu akichaguliwa kuwa rais wa nne wa Kenya.Maswala haya ni; Usalama wa Taifa, usalama wa chakula na miundombinu ya ajira, huduma za afya, elimu, utalii, kuboresha makazi duni, maji, kilimo, Waafrika wanaoishi ulaya, mazingira na viwanda.[9]

Ata mgombezi wa kwanza wa kiti cha urais amabaye hana jina la Kiafrika. Wakazi wa eneo mbunge la Gatanga katika siku za hapo awali walikuwa wanamwita muthungu (mzungu katika lugha ya kiswahili) kwa sababu ya kuwa yeye hukutana na kamati ya bunge ya Maendeleo saa 7:00 asubuhi.[10]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Anapenda Kilimo, Bima, biashara ya kujenga nyumba na Viwanda. Yeye pia ana mengi yanayomhusisha na michezo, baada ya kuwa mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya mnamo 1996 hadi 2000 na kuwa mwakilishi katika Kamati ya FIFA (futsal) kuanzia mwaka 1998 hadi 2000.Kenneth alikuwa kipa alipokuwa bado katika shule na hata alikwenda kucheza katika Ligi Kuu ya Kenya kwenye timu ya Reunion FC. Baadaye alilazimishwa kujiuzulu kutoka kucheza kandanda baada ya kuvunjika kwenye mkono wake wa kulia.[11]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
  1. "Peter Kenneth|Kenyans Decide". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-04. Iliwekwa mnamo 27 Mei 2012.
  2. "Peter Kenneth Profile and Biography". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-12. Iliwekwa mnamo 27 Mei 2012.
  3. "Peter Kenneth MP for Gatanga Constituency". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-12-16. Iliwekwa mnamo 27 Mei 2012.
  4. "Peter Kenneth (Kenya)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-09-05. Iliwekwa mnamo 27 Mei 2012.
  5. Gatanga Constituency Ilihifadhiwa 28 Desemba 2018 kwenye Wayback Machine.. Gatanga Constituency.
  6. "Jackal News : We own News and Gossip". thejackalnews.com. 8 Mei 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-18. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2012.
  7. Ndonga, Simon (7 Mei 2012). "Capital News » Gatanga still tops in proper CDF use". capitalfm.co.ke. Capital Broadcasting Network. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2012.
  8. Mureithi, Francis (12 Desemba 2012). "Peter Kenneth launches his 2012 manifesto". the-star.co.ke. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-01-12. Iliwekwa mnamo 16 Juli 2012. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  9. MUREITHI, FRANCIS (12 Desemba 2012). "Peter Kenneth launches his 2012 manifesto". the-star.co.ke. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-01-12. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2012.
  10. Opanga, Kwendo (13 Agosti 2011). "allAfrica.com: Kenya: Why Peter Kenneth is 'Mzungu' to Kabogo". allafrica.com. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2012.
  11. Otieno, Brian (26 Juni 2012). "allAfrica.com: Kenya: Kenneth Accuses State of Neglecting Sports". allafrica.com. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2012.