Peter Tabichi ni mtawa wa Shirika la Wafransisko na mwalimu wa hisabati na fizikia katika shule ya sekondari ya Keriko katika kaunti ya Nakuru nchini Kenya.
Ameshinda mwaka 2019 Tuzo ya Mwalimu Bora Ulimwenguni kutoka Shirika la Varkey (Varkey Foundation).
Alizaliwa mwaka 1982 katika kijiji kidogo cha Kenya. Peter Tabichi alipokuwa na miaka kumi na moja mama yake alifariki. Halafu, alilelewa na baba yake tu[1].
Alihamasishwa kuwa mwalimu kwa sababu watu wengi wa familia yake walikuwa walimu: baba yake, na baadhi ya wajomba na binamu zake[2]. Alitaka kutumia elimu kuwasaidia wanafunzi na familia zao.
Alisoma shahada ya kwanza Chuo kikuu cha Egerton katika Nakuru, Kenya[3]. Tabichi ni mtawa wa kanisa Katoliki[4]. Anatumia masuala ya dini kufundisha vizuri. Kazi yake ya kufundisha alianza katika shule ya binafsi.
Tabichi alifundisha hisabati, fisikia, na kemia katika Shule ya Sekondari ya Keriko, kijiji cha eneo la pwani, kutoka mwaka 2016. Hicho kijiji ni maskini, watu wengi hawana pesa na vyakula vya kutosha[5]. Kuna masuala mengi kama vile ujauzito wa vijana, kuacha shule mapema, uhaba wa vifaa vya elimu[6]. Asilimia tisini na tano ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Keriko wana umaskini. Tabichi amefanya kazi nyingi kuwasaidia wanafunzi wa kijiji. Tabichi hutumia asilimia themanini ya mshahara wake kuwalipia vitabu na sare wanafunzi wake[7].
Ameanza Klabu ya Kukuza Talanta na Klabu ya Imani shuleni[8]. Pia amechangia Klabu ya Sayansi. Wanafunzi wa Tabichi wamekamilisha vitu vingi. Baadhi ya wanafunzi wake wameshindana raundi ya mwisho ya Maonyesho Duniani ya Sayansi na Uhandisi ya Intel. Mmojawapo ameshinda tuzo ya Royal Society ya Kemia[9]. Tabichi aliposhinda Tuzo ya Mwalimu Bora Ulimwenguni, ameuambia umma kwamba anataka kutumia tuzo ya dola milioni moja kuwatumia wanafunzi wa Kijiji cha Pwani na shule yao.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Peter Tabichi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |