Piotr Balcerzak

Piotr Balcerzak (alizaliwa Warshawa, 25 Juni 1975) ni mwanariadha wa zamani wa mbio fupi kutoka Polandi. Alipata mafanikio makubwa zaidi akiwa na timu ya Polandi ya mbio za kupokezana vijiti za mita 4 x 100.

Ameoa mwanariadha mwenzake wa Poland, Joanna Niełacna.