Prednicarbate, inayouzwa kwa jina la chapa Dermatop miongoni mwa zingine, ni kotikosteroidi inayotumika kutibu magonjwa ya ngozi kama vile ugonjwa wa ngozi wa atopiki, hali ya seli za ngozi kujijenga na kutengeneza mabaka makavu na yanayowasha (psoriasis), na ugonjwa wa ngozi unaotokana na mguso.[1] Dawa hii inatumika kwa ngozi.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuungua, kuwashwa, kukonda kwa ngozi, chunusi, kupoteza rangi, michirizi ya ngozi (striae) na hali ya mtu kuwa na mishipa midogo ya damu iliyopanuka karibu na sehemu ya juu ya ngozi (telangiectasia).[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha maambukizi ya ngozi, athari za mzio na ugonjwa wa Cushing.[1] Dawa hii inachukuliwa kuwa steroidi ya nguvu ya kati.[1]
Prednicarbate iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1991[1] na inapatikana kama dawa ya kawaida.[2] Bomba la gramu 60 nchini Marekani linagharimu takriban dola 34 za Marekani kufikia mwaka wa 2021.[2]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Prednicarbate kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |