Raam Daan

Raam Daan ni bendi ya mbalax kutoka Senegal. Ilianzishwa mnamo mwaka wa 1974 na Thione Seck, Raam Daan ameweza kuwa mojawapo ya bendi maarufu zaidi za mbalax nchini Senegal (ikishindanishwa tu na Youssou N'Dour & bendi yake ya Super Etoile de Dakar).

Jina la "Raam Daan" linamaanisha, "kufikia lengo lako" katika lugha ya Wolof.

Thione Seck anabainisha mbalax ya Raam Daan kama "safi na yenye nguvu." Ala ya Raam Daan inajumuisha kibodi 3, gitaa, gitaa la besi, seti ya ngoma na ngoma za sabar.[1]