Ramez Naam

Ramez Naam ni mwanateknolojia na mwandishi wa hadithi za kufikirika wa Marekani.

Anajulikana zaidi kama mwandishi wa Nexus Trilogy. Vitabu vyake vingine ni pamoja na The Infinite Resource: The Power of Ideas on a Finite Planet na More than Human: Embracing the Promises of Biological Enhancement. Kwa sasa ni mwenyekiti mwenza wa nishati na mazingira katika Chuo Kikuu cha Singularity.[1]

Hapo awali, Naam alikuwa mwanasayansi wa kompyuta Microsoft kwa miaka 13, na aliongoza timu zilizofanya kazi kwenye Outlook, Internet Explorer, na Bing.[2]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Naam alizaliwa Cairo, Misri, katika familia ya Kikristo ya Kikopti[3] na alikuja Marekani alipokuwa na umri wa miaka mitatu. Alifanya kazi kama mwokozi wa majini.[4] Naam alikuwa mwanasayansi wa kompyuta Microsoft kwa miaka 13, na aliongoza timu zilizofanya kazi kwenye Outlook, Internet Explorer, na Bing.[1]

Ramez Naam ni Profesa Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Singularity, ambapo anafundisha juu ya nishati, mazingira, na uvumbuzi. Ameonekana katika kipind cha jumapili asubuhi MSNBC, Yahoo! Finance, China Cable Television, BigThink na Reuters.fm. Kazi zake zimeonekana, au imepitiwa upya na, The New York Times, The Wall Street Journal, Los Angeles Times, The Atlantic, Slate, Business Week, Business Insider, Discover, Popular Science, Wired na Scientific America. [5]

Kitabu cha Naam Nexus kilikuwa mojawapo ya vitabu bora zaidi vya NPR mwaka 2013.[6] Nexus na mwendelezo wake huchunguza hatari na zawadi zinazowezekana za teknolojia inayowaruhusu wanadamu kuunganisha mawazo yao moja kwa moja.[6]

Mnamo 2005 alipokea Tuzo la H.G. Wells kwa Michango ya Transhumanism.[7]

Mnamo 2014 Nexus ilishinda Tuzo ya Prometheus, na aliteuliwa kwa Tuzo ya John W. Campbell kwa Mwandishi Bora Mpya.[8] Mnamo 2015 Apex alishinda tuzo ya Philip K. Dick.[9]

  1. 1.0 1.1 Frank Catalano (2018-02-13). "Scaling to optimism: Futurist, author and computer scientist Ramez Naam on the power of cheap tech". GeekWire (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-09-29.
  2. Frank Catalano (2018-02-13). "Scaling to optimism: Futurist, author and computer scientist Ramez Naam on the power of cheap tech". GeekWire (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-09-29.
  3. Ramez Naam (2013-01-10). "The biggest problem with Egypt's new constitution is that it will probably be ignored". Quartz (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-09-29.
  4. "Ramez Naam". www.goodreads.com. Iliwekwa mnamo 2022-09-29.
  5. Socrates (2014-01-20). "Science Fiction Author Ramez Naam: The Future Isn't Set In Stone!". Singularity Weblog (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-09-29.
  6. 6.0 6.1 Frank, Adam (2016-08-02), "Nexus: Choosing Sides In The Trans-Human Revolution", NPR (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2022-09-29
  7. Alex Pearlman. "Home". IEET (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-09-29.
  8. "2014 Hugo Awards". The Hugo Awards (kwa American English). 2014-04-18. Iliwekwa mnamo 2022-09-29.
  9. "Ramez Naam's Apex Is The Winner Of The Philip K. Dick Award". Gizmodo (kwa American English). 2016-03-26. Iliwekwa mnamo 2022-09-29.