Rimegepanti (Rimegepant), inayouzwa kwa jina la chapa Nurtec ODT, ni dawa inayotumika kutibu na kuzuia kipandauso.[1] Inachukuliwa kwa mdomo.[2] Huanza kazi ndani ya masaa mawili na athari zake zinaweza kudumu kwa masaa 48.[3]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu na maumivu ya tumbo.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito na kunyonyesha hauko wazi.[4] Dawa hii inafanya kazi kwa kuzuia kipokezi cha CGRP.[2]
Rimegepanti iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2020.[2] Nchini Marekani, inagharimu takriban dola 120 za Marekani kwa kila dozi kufikia mwaka wa 2021.[5] Kufikia mwaka wa 2021 ilikuwa bado haijaidhinishwa Ulaya wala Uingereza.[6]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rimegepanti kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |