Ronald Baecker

Ronald Baecker (amezaliwa Oktoba 7, 1942) ni profesa wa sayansi ya kompyuta aliyeshika nafasi iliyofadhiliwa na taasisi ya Maabara ya Bell kwenye chuo kikuu cha Toronto. Alifanya utafiti hasa kuhusu mifumo ya muingiliano kati ya kompyuta na binadamu[1] Ni mwanzilishi muandamizi wa mradi wa Dynamic Graphics, na muanzilishi wa Taasisi ya Knowledge Media Design, Maabara ya Gracefully Ageing Technologies (TAGlab)[2]. Ni mwandishi wa kitabu kilichochapishwa mwaka 2019 na Chuo Kikuu cha Oxford kiitwacho Kompyuta na Jamii: Mtazamo wa kisasa ("Computer and Society: Modern Perspectives" ) na mwandishi muandamizi wa "COVID-19 Solutions Guide" kilichochapishwa mwaka 2020,na pia alichapisha mwenyewe "Digital Dreams Have Become Nightmares: What We Must Do in 2021".[3]

  1. "Ron Baecker, Ronald Baecker". scholar.google.com. Iliwekwa mnamo 2022-09-09.
  2. "Dr. Ron Baecker's Home Page". ron.taglab.ca. Iliwekwa mnamo 2022-09-09.
  3. "Ronald M. Baecker". www.amazon.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-09-09.