Roselina (1263 – 17 Januari 1329) alikuwa kiongozi wa monasteri ya Kikartusi ya Celle-Roubaud, karibu na Fréjus, mkoa wa Provence, leo nchini Ufaransa, aliyeng’aa kwa kujinyima, kufunga chakula, kukesha na kushika maisha magumu kwa jumla[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa katika tarehe ya kifo chake[2][3].