Samar (Filamu ya 2013)

Samar ni filamu ya lugha ya Kitamil ya India ya mwaka 2013, yenye hadithi ya kutatanisha na vitendo vya ujasusi-vitisho ilivyoandikwa na kuongozwa na Thiru.[1]Imeigizwa na wasanii kama Vishal, Trisha, na Sunaina, huku Manoj Bajpayee na J. D. Chakravarthy wakiwa kama wasanii wasaidizi.Richard M. Nathan alihusika na upigaji picha, wakati sauti na alama za filamu zilikamilishwa na Yuvan Shankar Raja na Dharan Kumar.[2] Baadaye, ilidubuwa kwa Kihindi kama "Gabbar Sher" mnamo 2016.Hadithi inazungumzia mwogoza wapanda milima, ambaye analazimishwa kuondoka kwenda Bangkok chini ya mazingira ya ajabu na anashuhudia mfululizo wa matukio ya kushangaza huko. Baada ya kucheleweshwa mara kadhaa, hatimaye filamu ilizinduliwa tarehe 13 Januari 2013.[3]

  1. BBFC. "Samar". www.bbfc.co.uk (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-04.
  2. "Dharan does it for Yuvan !, Samar, Dharan Kumar". www.behindwoods.com. Iliwekwa mnamo 2024-05-04.
  3. "Strange encounters", The Hindu (kwa Indian English), 2012-07-14, ISSN 0971-751X, iliwekwa mnamo 2024-05-04
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Samar (Filamu ya 2013) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.