Sediqa Balkhi (alizaliwa 1950) ni mwanasiasa wa Afghanistan na alikuwa Waziri katika serikali ya Hamid Karzai.[1]
Balkhi alizaliwa mnamo mwaka mwaka 1950 mjini Mazar-i-Sharif, Mkoa wa Balkh, Afghanistan. Baba yake, Ismael Balkhi, alifungwa jela mara kadhaa nchini Afghanistan na hatimaye akapewa sumu.[2] Alipata shahada yake ya B.A. katika Masomo ya Kiislamu na kuendelea na elimu zaidi alipokuwa Iran. Alifundisha kwa muda na kufanya kazi kama meneja.[3] Aliolewa akiwa kijana na alikuwa na watoto sita. Ndugu yake, Seyyed Ali Balkhi, alikuwa mchumi ambaye aliuawa wakati wa utawala wa chama cha kikomunisti cha Watu wa Kidemokrasia wa Afghanistan.[2]
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sediqa Balkhi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |