Segun Arinze (Segun Padonou Aina; alizaliwa 1965 [1]) ni mwigizaji na mwimbaji wa Nigeria.[2][3][4][5][6]
Segun alizaliwa Onitsha, jimbo la Anambra na baba wa kabila la Yoruba na mama wa kabila la Igbo. Ni mzaliwa wa Badagry, jimbo la Lagos. Alihudhuria Victory College of Commerce huko Ilorin, kisha akaenda Taba Commercial College iliyopo jimbo la Kaduna baada ya kumaliza elimu yake ya shule ya upili.
Alisomea Michezo ya Kuigiza katika Obafemi Awolowo University. Anafahamika almaarufu kama Black Arrow ambapo alipata jina hilo katika uhusika alioigiza.[7]
Alimuoa mwigizaji mwenzake wa Nollywood Anne Njemanze, ambae baadaye alikuja kuwa na maisha ya ndoa mafupi kuliko alioyaishi.[8] Wanandoa hao walikua na binti mmoja, Renny Morenike, aliyezaliwa tarehe 10 Mei.[9]
Alianza uigizaji ndani ya Ilorin. Mbali na uigizaji, Segun pia ni mkufunzi wa waigizaji na kwa sasa anafanya kazi na African international film festival kwa kutoa maarifa kwa kizazi kijacho cha waigizaji.[10][11][12]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Segun Arinze kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |