Shule ya Brookhouse

Brookhouse

Shule ya Kimataifa ya Brookhouse iko katika kitongoji mjini Nairobi, karibu kilomita 14 kutoka katikati ya jiji. Shule hii ilifunguliwa mnamo mwaka wa 1981 na sasa ina shule ya chekechea, ya msingi na ya upili. Kuna bweni malazi kwa wanafunzi 150. Vifaa vya michezo vilivyomo ni kama bwawa la kuogelea na nyanja za kuchezea mpira, mpira wa raga na kriketi Shule hii iko karibu na Mbuga ya wanyama ya Nairobi na eneo kubwa la mbuga hii inaweza kutizamwa kutoka kwa bweni ya wanafunzi.

Vifaa katika Shule ya Brookhouse, jijini Nairobi, ni: maabara tatu zilizojengwa kwa madhumuni ya kutumika kisayansi, maktaba mpya, vyumba 3 vya kompyuta, chumba cha kufanya mazoezi, jukwaa la kisasa na kituo cha kidato cha sita.

Shule hii inatoa mfumo wa michezo ya ziada ikiwemo michezo tofautitofauti pamoja na safari. Shule hii hutumia mfumo wa masomo ya Taifa ya Kiingereza na wanafunzi kufanya mtihani wa N.C. wakiwa na umri wa miaka 7, 11 na 14, na mtihani wa IGCSE wakiwa na umri wa 16 na 'A' Level wakiwa na miaka 18. Wanafunzi wengi hujiunga na vyuo vikuu vilivyo nchini Uingereza, lakini ongezeko la idadi ya wanafunzi wameanza kwenda nchi za Marekani, Australia na Afrika ya Kusini. Shule hii hutoa ESL na msaada wa kidharura. Wanafunzi wote wa sekondari hufanya kazi ya huduma ya jamii isiyo chini ya masaa 50 kila mwaka na pia hushindana mashindano tofauti tofauti kati ya timu za shule.

Madarasa katika shule hii ina wastani wa wanafunzi 16, na hakuna zaidi ya wanafunzi 20 katika darasa lolote. Wanafunzi wa shule hii hutoka kwa mataifa thelathini na mbili, ingawa wateja wakuu ni watoto wa wafanyibiashara na jumuiya za wanadiplomasia mjini Nairobi.

Kujiunga kwa mwanafunzi yoyote ni kwa kufanya mtihani wa kiingilio na/au kutumia ripoti za shule ya awali. Kujiunga kwa A-Level hutegemea matokeo na mafanikio ya IGCSE

Shule hii ilichaguliwa na Good Schools Guide International[1].

  1. http://gsgi.co.uk/countries/kenya/nairobi/kenyan-schools-considered-by-expats

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]