Shule ya Upili ya Wavulana ya Starehe (maarufu kama "STAREHE") ni shule ya bweni na kutwa, ya wavulana pekee, katika eneo la Nairobi, Kenya.
Shule ilianzishwa mwaka 1959 na Geoffrey William Griffin, MBS, OBE, Geoffrey Gatama Geturo na Joseph Kamiru Gikubu. Ilianza kama kituo cha kuwaokoa watoto. Starehe na Shule ya Brookhouse ni shule za pekee za Kiafrika kusini kwa Sahara na kaskazini kwa mto Limpopo zinazotambulikana kama wanachama wa Round Square.
Starehe imeelezewa na BBC kuwa labda shule bora nchini Kenya.[1]
Shule ya Upili ya Wavulana ya Starehe ni ya kipekee kati ya shule za Kenya huru kwa sababu asilimia 70 husoma bila malipo, na wale wengine hulipa kiwango cha chini cha karo. Hili linatokana na makubaliano ya uasisi wake kama shule ya hisani. Karo ya shile hulipwa kutokana na mapato ya mzazi, huku shule ikigharamia kiasi fulani, ili wanafunzi kutoka matabaka tofauti ya jamii wapate masomo ya umma yaliyo makamilifu, ya hali ya juu, high-quality, ambayo labda yangekuwa zaidi ya uwezo wao kimapato.
Mchakato wa kuingia shuleni huanzia na kupokelewa kwa matokeo ya mtihani wa kitaifa KCPE na hupendelea kuteua wanafunzi ambao wanaonyesha uwezo wa kufaidika kielimu kutokana na mazingira mufti ya shule hii.
Shule hii huendeshwa na Kamati Kuu ambayo mwenyekiti wake ni Patrick Obath, aliyekuwa Mkurugenziwa kampuni ya wa Kenya Shell and BP, wathamini wakuu wa shule hii tangu ilipoanzishwa.
Hitaji la kuhakikisha mustakabali wa shule hii kwa sasa unashughulikiwa na waliokuwa wanafunzi wa shule hii pamoja na Raios wa nchi ya Kenya na marafiki wa dhati pamoja na wanaojitolea.
Kuteuliwa kuingia shuleni ni kwa mashindano huria katika mtihani. Wanaotaka kujiunga na shule hii hujaza "Fomu za Manjano" kabla ya tarehe 31 Julai katika mwaka unaotangulia mwaka wanaotaka kujiunga na shule. Kila mwaka, takriban maombi 20,000 hupokelewa na ni wanafunzi 210 tu wanaoteuliwa kujiunga na wanafunzi wengine na takriban nafasi 6 huachwa kwa ajili ya wanafunzi wasiojiweza kabisa ambao huenda hawakuwa na nafasi ya kutuma maombi lakini wakaupita mtihani.
Wanaotuma maombi huteuliwa kulingana na mapato ya wazazi na matokeo yao katika mtihani wa kitaifa wa KCPE. Uteuzi unategemea matokeo haya tu.
Shule ya Upili ya Wavulana ya Starehe ilikuwa ni matokeo ya maono ya Geoffrey William Griffin, akisaidiwa na Joseph Gikubu, na Geoffrey Geturo. Mwanzo wake ilikuwa hali ya hatari iliyotangazwa na Gavana wa kikoloni Kenya wakati wa mapambano ya Mau Mau mwaka 1952 kulikosababisha kufurika kwa mayatima maskini na wasiokuwa na makao mitaani.
Wavulana 17 wa kwanza waliingia shuleni kutoka Kituo cha Kuokua Watoto cha Karikor, Nairobi, na shule yenyewe ilikuwa katika vibanda viwli vya mabati vilivyoruzukiwa na kampuni ya Shell and BP mwaka 1959. Baada ya miezi michache shule ilihamia eneo lake la sasa, Starehe, Nairobi.
Jina "STAREHE" ni neno la Kiswahili lenye maana ya 'Utulivu', 'Amani', au 'Faraja', likimaanisha mahali ambapo wavulana yatima wangeweza kupata furaha katika msingi wake wa kikabwela. Pia ni jina la mahali ambapo shule hii ipo.
Shule hii ni mwanachama wa Roundsquare shirika la kimataifa la shule zinazotoa elimu kwa wanafunzi kutoka matabaka mbalimbali, wengi wakiwa maskini.
Shule hii inajulikana mno kwa sababu ya sare yake: maarufu kama 'Red na Blue',kaptula ya buluu na shati jekundu, zinazovaliwa na tai nbyeusi na bleza au sweta ya kizibau.
Mwingiliano na jamii pamoja na kushikamana na nchi huzingatiwa, huku kila likizo ya mwezi ikitumika kwa ajili ya huduma za bure kwa jamii katika hospitali, zahanati au afisi za serikali au katika asasi nyingine yoyote ambayo wanafunzi wanapendekeza. Huduma hii inafahamika kama Voluntary Service Scheme, na ni njia ya kuishukuru na kuiauni jamii.
Starehe huwa na mechi ya kisasi dhidi ya shule ya Lenana kabla ya Dhifa ya Jioni ya Waanzilishi.
Kila asubuhi ili kukaribisha mwanzo wa siku ya masomo, kila jioni kumaliza siku ya masomo, na kila wakati bendi ya shule inahitaji mkutano wa wanabendi wake, baragumu inayohusika hupigwa na mtaalam wa kazi hiyo kutoka kwenye bendi ambaye hupata uluwa fulani kutokana na nafasi yake. Mifano ya uluwa ni pamoja na kutembea kwenye barabara kuu za shule badala ya kukimbia kama wengine Starehe na kupata kibali cha kutohudhuria gwaride la kawaida kama wengine.
Shule ya Upili ya Wavulana ya Stareheina. Hili limekuwa dhahiri katika ushindi mwngi katika Tamasha za muziki nchini Kenya unaofanyika kila mwaka nchini. Mafanikio yamekuwa katika ngazi za kibinfasi na katika ngaziya shule kwa jumla.
Kanisa la shule lina viti 1,000 pamoja na piano kubwa , iliyo moja kati ya piano mbili kubwa zilizo shuleni (nyingine ikiwa kwenye ukumbi wa mikutano). Kwaya ya shule imefanikiwa imefanya mafanikio mengi na hivyo ana sifa yachuma ni bora. Katika historia ya shule,wanafunzi wengi wenye vipawa vya kimuziki wamefanikiwa katika mashindano ya kibinafsi na mitihani na kuacha taathira kubwa katika jamii ya kimuziki ya Kenya. Baadhi yao ni wanachama wa Okestra ya mji wa Nairobi.
Shule hi ina kwaya nyingine nyingi ndogo na mipangilio ya ala za muziki, pamoja na sherehe ya kila mwaka House Singing Competition kuitwa "Interhouse Halisi Gala", uliofanyika tarehe ya mwisho usiku wa shule ya kwanza ya muda mrefu. Idara ya Muziki hupangilia matamasha haya kila mwaka, kutoa fursa kwa kuchipuka kwa vipawa vya kimuziki.
Hii ni bendi maarufu kitaifa, na imepata sifa za kimataifa, baada ya kucheza katika taasisi mbalimbali na kutumbuiza katika maadhimisho ya kitaifa. Bendi hi iliongoza maandamano ya mazishi ya Dk Griffin mwaka 2005.
Historia ya muziki saa Starehe ni mkono na marafiki wa Starehe pamoja. Shirika hili lipo nchini Uingereza na hutuma walimu wawili wa muziki wa kujitolea kila mwaka kuja Starehe. Shirika hili pia huwaalika wanafunzi kutoka Shule ya wasichana ya Starehe na Shule ya wavulana ya Starehe kutuimbuiza hadhira nchini Uingereza.
Ingawa kuna tetesi nchini kwamba malazi ya hapa ni ya starehe, hili si jambo la kweli. Wanafunzi huoga maji baridi, kawaida ya shu. Elimu ya Starehe husisitiza ufanisi wa kielimu, kuwajibika na nidhamu. Maandishi kwenye mlango wa Ukumbi wa Mikutano husoma hivi: The path of duty is the way to Glory (Njia ya Wajibu ni njia ya Utukufu). Wanafunzi wanahitajika kutekeleza majukumu ya kila siku ambayo ni pamoja na kusafisha mabweni yao na shule vile vile maeneo yanayozunguka mabweni, madarasa na maabara. Hili hasa hutendeka katika ngazi ya kidarasa na kulingana na kidato.
Starehe hufuata cheo makao mfumo gavana kulazimisha high nidhamu viwango kwa mwanafunzi wake wa mwili. Mwanafunzi anaweza kuwa kiranja tu kuanzia mwaka wa pili shuleni. Hata hivyo, wao hawawi viranja kamili kamwe. Wao huwa na daraja la kiranja-mdogo hadi Mkurugenzi anapotangaza kupandishwa kwao madaraka. Kupandishwa madaraka kupitia ngazi za daraja hutegemea hulka na kuwajibika, ambako hutathminiwa na Viranja wa Shule (ambao hujulikana kama Makapteni wa Mabweni) ambao huunda Jopo la Viranja Wakuu wa Shule. Yeyote anayependekezwa kuwa kiranja huchuchung Maamuzi mengi hutegemea kupigwa kura na kuchaguliwa kwa pendekezo la wengi. Hata hivyo, mamlaka yan kumteua au kumwachisha kazi kiranja ni ya Mkurugenzi tu, ambaye hupewa mawaidha na Jopo la Viranja Wakuu.
Kiranja Mkuu na manaibu wake wawili mara nyingi inafahamika kama 'Red Lions'. Manaibu wawili ni sawa katika cheo. The House Viranja Wakuu kuchukua malipo ya bweni 12 ya nyumba na idara nyingine katika shule kama vile maktaba, michezo idara, Chapel na mkutano. Kila bweni huchukuliwa kuwa nyumbani kwa mwanafunzi katika miaka yake yote minne akiwa shuleni. Hapa, atakuwa akifanya urafiki na mwamana utakaomwelekeza na kumdumisha katika maisha yake yote Starehe. Mara nyingi, wanafunzi huelekea kujihusisha sana na mabweni yao hata baada ya kuondoka. Chini ya Vijanja wadogo, kuna wanafunzi wa kawaida au 'commoners' Viranja hutambulika vifuatavyo kulingana na madaraka yao:
- Kapteni wa Shule- Nembo ya Simba Mwekundu juu ya Utepe za shaba kwenye koti.
- Naibu wa Kapteni wa shule - Pia huwa na nembo ya simba mwekundu lakini huw ana Utepe moja kwenye koti.
- Viranja wa Mabweni - Pini ya dhahabu ya Nembo ya Simba.
- Kiranja mwandamizi - Pini ya dhahabu yenye nembo ya nyota.
- Viranja- nembo(kijivu kuvuka bakora).
- Viranja wadogo
Kupanda kimadaraka kunaonyeshw akwa kutuzwa kwa nembo na pini zilizo hapo juu. Hizi huvaliwa upande wa kulia wa mkono wa koti .
Wasio na madaraka hugawanyika kulingana na mwaka waliojiunga na shule. Wale walio katika Kidato cha Kwanza na cha pili huitwa Wavulana Vijulanga na wale wa kidato cha tatu na nne ni Wavulana Wakomavu. Starehe ina viwango vya juu vya nidhamu vinavyotekelezwa na mfumo mwafaka wa adhabu na hutofautiana kwa ukali kulingana na kosa lililotendwa. Walimu, Wafanyikazi wenye malaka ya kiutawala na viranja wanaruhusiwa kuwapa adhabu wanafunzi. Mwanafunzi ambaye anahisi kuwa yeye ameadhibiwa kimakosa na kiranja anaweza kukata rufaa kwa mwanafunzi juu rasmi. Hata hivyo, lazima afuate ngazi za mamlaka. Adhabu hizi kwa ujumla huhusisha kazi za mikono. Kama kanuni ya jumla, adhabu inayotolewa na mwalimu haina rufaa ila kuwe na sababu nzuri sana. Rifaa kama hizi hutolewa na Mwalimu Mkuu.
Wakati adhabu ya viboko ilikuwa ingali imeruhusiwa nchini Kenya, ni Mkurugenzi tualiruhusiwa kutumia miwa saa Starehe. Hii ilikuwa ili ajue makosa makubwa yaliyotendeka shuleni.[2]
Dkt. Griffin alitofautiana na serikali kuhusu kupiga marufuku matumizi ya kiboko shuleni, akitaja kwamba serikali ilikuwa ikikubali shinikizo la kimataifa bila kufikiria kwa kina matokeo yake. Alisema kwamba hilo lingesababisha kuongezeka kwa ukosefu wa nidhamu na kushusha kiwango cha elimu.
Mabweni ya Starehe yamepewa majina kulingana na waruzuku wakuu katika nyakati mbalimbali pamoja na watu maarufu katika historia ya Kenya wanaohusika na shule hii.
Kuna mabweni 12 ambayo wanafunzi wapya huingizwa kila mwaka:
- Gikubu - jina la mwanzilishi-mwenza Joseph Gikubu
- Ngala - jina la marehemu Ronald Ngala, waziri katika serikali ya Jomo Kenyatta
- Geturo - jina la mwanzilishi-mwenza Geoffrey Gatama Geturo
- Shaw House - jina la marehemu Patrick David Shaw, afisa mkuu wa polisi wa kutisha aliyewaondoa wezi na wanyang'anyi jijini Nairobi. Alikuwa msaidizi wa Mkurugenzi wa Starehe akihusika na maswala ya utawala hadi alipoaga dunia.
- Horsten - jina la marehemu Balozi wa Kideni aliyekuwa mruzuku mkuu wa shule.
- Mboya - jina la marehemu Thomas Joseph Mboya aliyekuwa mlezi wa shule na waziri mtukuka katika serikali ya Jomo Kenyatta
- Shell - jina la mruzuku mkuu wa Starehe tangu kuanzishwa kwake,kampuni ya mafuta ya Shell-BP
- Chaka - jina la shujaa maarufu na mfalme wa Kizulu Shaka Zulu.
- Njonjo - jina la aliyekuwa Mkuu wa Sheria, waziri wa Haki na Maswala ya Kikatiba katika serikali za Jomo Kenyatta na Daniel Arap Moi Toroitich, Charles Njonjo.
- Kirkley - jina la rafiki wa Starehe, Sir Lesley Kirkley
- Muriuki - jina la mmojawapo wa wanachama waliohudumu kwenywe Halmashauri ya Shule kwa muda mrefu sana, Nick Muriuki Mugwandia
- Kibaki - jina la mlezi wa Shule tangu mwaka 1969 na Rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya Mh. Mwai Kibaki
Mmojawapo wa nyimbo za Starehe (Forty Years On) umeandikwa kutokana na wimbo rasmi wa shule ya Harrow.
1 These are the years when we are helped and guided
Taught by Starehe to know and judge and do;
Prepared for the future, encouraged and provided,
Strengthened to serve: Natulenge Juu!
2 Brought to the school to join a thousand others
All with one purpose, quick and keen and true;
Boldy we follow in the footsteps of our brothers,
Proudly we wear our dress of red and blue.
3 Honour the School, a way of life which fires us,
Lifts up our spirits, sets us all ablaze,
Teaches and trains, rebukes and inspires us,
Planting the seed to serve us all our days.
4 We pledge ourselves, when this our generation
Must in its turn the weight of government bear,
To all mankind, through service to our nation,
Head, heart and hand in justice, zeal and care.
5 These are the years when we are helped and guided
Taught by Starehe to know and judge and do;
Prepared for the future, encouraged and provided,
Strengthened to serve: Natulenge Juu!
Baadhi ya misimu ya Starehe hufanana na za shule nyingine lakini hutofautiana kwa namna fulani. Orodha ifuatayo huenda si kamilifu lakini inaonyesha simo ambazo wanafunzi wa Starehe hutumia katika mazungumzo.
- Boss: njia ya kijanja ya kumwita Mkurugenzi. Hata hivyo, kwa baadhi ya wanafunzi, mtajo wa jina hilo unaleta mizizimo. Licha ya hayo, jina hilo linaonyesha heshima ya dhati.
- Cop (s) (Kopa/Makopa, Karao/Makarao): kiranja/viranja
- To get Fixed (Kufiksiwa): kuahidiwa kupata adhabu.
- Murram: pure ni chakula cha kawaida cha Chumba cha Maakuli, kinachotayarishwa kuwa kama kokoto za barabarani. Pilipili huongeza ladha katika murram.
- A Cheque (Cheki): kibarua chenye maandishi anachopewa nliyefanya kosa na mwenye mamlaka. Kinaweza "kupokezwa hela" baada ya anayeandikiwa kukitia sahihi; na baada ya adhabu kutendeka. Kwa mfano wa mwalimu ana uwezo wa kuandika mwanafunzi yoyote Cheki kwa Mwalimu Msimamizi wa Kidato (au Mkurugenzi) kwa sababu yoyote - kama vile kukosa kumakinika darasani.
- Rabble (Rabo): mwanafunzi wa kidato cha kwanza ambaye anahitajika kujua wimbo wa shule na wimbo wa Forty Years On katika wiki kadhaa za mwanzo. Cop anaweza kumwambia Rabblekuimba wimbo wa shulke, (kwa mfano aya ya 3) na akishindwa atapata adhabu. Marabble hukimbia kuelekea katika Ukumbi wa Mikutano kwa ajili ya gwaride la jioni na kukaa kwenye fomu za mbele ilihali wanafunzi wa vidato vya juu hutembea kuelekea Ukumbini na kukaa kwenye viti vya nyuma. Wanafunzi wa vidato vya juu pia huondoka ukumbini kabla ya marabble. Pia, Wanafunzi wa vidato vya juu hupewa chakula mwanzo katika Chumba cha Maakuli. Rabbles pia kuvaa kaptula, kwenda kwa katika mazoezi baada ya gwaride na kulala saa 3:30 usiku; baada kipindi cha kusoma kwa ziada. Kuteswa kwa namna yoyote au ni namna ungentlemanly tabia na wala inatekelezwa wala kuruhusiwa, sembuse condoned.
- Across: upande mwingine wa shule kubwa ambapo wanafunzi wa vidato vya juu huwa na masomo yao. Wanaweza kujipumziosha katika uwanja wakati wa mapumziko.
- Starehe Forest: kisitu kidogo sehemu ya Across karibu na eneo la riadha. Baadhi ya wanafunzi hudhani ni salama 'kwa faragha' lakini wamekuwa wakigundulika mara kwa mara na viranja waangalifu.
- Mining (Kumine): Kusafisha vyoo, jukumu walilotengewa Marabble.. Hata hivyo, wanafunzi wenye tabia mbovu wa vidato vya juu wanaweza pia kupewa 'Madini Duty'.
- To be Pushed (Kusukumwa): Huku hakutamaniki. Ni kuletwa mbele ya Mkurugenzi kwa ajili ya suluhisho la haraka. Kwa mfano, mwanafunzi wa muziki ambaye haendi kufanya mazoezi bila sababu maalum anaweza kusukumwa kwa Boss. Katika nyakati za kitambo, huku kulikuwa pamoja na kupigwa viboko.
- Campaigner: jina la kejeli la kumwita mwanafunzi anayejipendekeza na hivyo kuutatiza udugu. Kwa mfano, anayeuliza maswali ya kipuzi darasani ili atambulike na mwalimu akijua vyema kwamba kengele ya kishuka iligonga dakika tano zilizotangulia.
- Baraza: kikao kama cha Bunge ambako malalamishi, matakwa, pongezi na masuala ya shule yanaweza kutolewa, kujadiliwa na suluhisho kutafutwa kwa kufuata itifaki ya kidiplomasia. Huhitimishwa kwa wimbo pamoja na piano, vinubi au ala nyingine za muziki za kupulizwa.
- Mugumo stump (Mugumo): mti unaofikiriwa kuwa mtakatifu katika kabila la Wakikuyu. Hupatikana sehemu moja ya uwanja wa jumuia na huwa mahali pa mikutano mingi ya dharura. Kwa sasa, kisiki hicho kimesogezwa hadi kwenye Uwanja wa "First Eleven" na sehemu hiyo sasa inajulikana kama "Palipokuwa Mugumo Stump"
- Tukutane baada ya Bugles: Baada ya gwaride, bendera ya shule hushushwa kufuatia muziki wa baragumu (kila mtu akiwa wima) Kwa hivyo, mtu akikwambia kwamba mkutane baada ya Bugles, maana yake ni kwamba umwone baada ya Gwaride.
!). Viranja hupendela kusema hivi kumtisha mwanafunzi asiye na cheo kumpeleka kwa Boss.
- sodi (sodium): anayeogopa kuoga maji baridi (akiogopa kuyeyuka).
- Kwenye Patrol: kuwa nje ya shule bila ruhusa (yaani kutokuwepo bila idhini). (Ni kosa kubwa sana).
- Lion/Simba: Kiranja anayehusika na usafi. Huogopwa sana na anaweza kuwaamuru hata wanafunzi wa vidato vya juu kufagia barabara.
- Kunyoa /Kushave: kutopewa kiwango cha chakula au alama unachostahili. Kwa mfano,ni kawaida kwa walimu 'kunyoa' alama kwenye insha bora - ambayo kuishia na alama ya takriba asilimia 60% chini. Hutumika kwa chakula katika Chumba cha Maakuli vile vile.
- Rec Room: Chumba cha mapumziko kwenye kila bweni ambapo wanachama wote wa bweni wanaweza kucheza tenisi, kutazama runinga (wikendi tu), kupiga pasi, kufanya mikutano n.k.
- Kukatia/Kuhook: Hali ya kuweza kumshawishi msichana anapoitembelea shule yenu.
- Kuslice/Kuhijack: Kunyang'anywa msichana uliyekuwa umehook.Unaweza pia kusema ume "De-hook".
- Weapon/Silaha: kijiko kinachotumika kulia (baadhi ya wanafunzi huvibeba mifukoni).
- Kuosha DH: mojawapo ya adhabu. Inahusisha kiranja kunyunyizia kiwango kikubwa cha sabuni kwenye sakafu ambayo utasugua na kisha kupiga deki kisha atatazama kabla ya kukuruhusu kukamilisha adhabu hiyo. Starehe hung'ara daima.
- Working Party: kikosi cha wanafunzi kwenye adhabu hii ambao hufanya kazi alasiri nzima ya Jumamosi. Kwa mfano, kukusanya nyasi (zilizokatwa majuzi na trekta) katika makundi ni adhabu ya kawaida ya Working Party ya Kwanza ya muhula - ambayo mara nyingi hupewa wale wanaoingia shuleni wakiwa wamechelewa bila sababu mahsusi.
- Drill/Drili: aina nyingine ya adhabu ambayo inahusisha kufanya mazoezi magumu ya viungo vya mwili. Husimamiwa na kiranja na hufanywa Jumanne na Alhamisi wakati wa mapumziko - mara nyingi ikiwa na hadhira kubwa.
- Drili Maalumu: Ni drili (tazama juu) ngumu kuliko ya kawaida na si rahisi kufanyika. Kutokana na uzito wake, inasimamiwa na Viranja Wakuu. Hupewa kikundi cha wanafunzi ambao mmoja ametenda kosa lakini wanamkinga. Miungano ya namna hiyo huleta "Tabia za Kiumati" ndiyo sababu huwa kali, ingawa inajulikana pia kwamba kuwadumba wenzako si tabia ya kiungwana.
- Stripe: Utepe mwekundu unaotuzwa baada ya kukamilisha mafunzo ya kuogelea unaowekwa kwenye nguo ya kuogelea. Ni lazima kuogelea kila wikendi hadi utakapopata utepe huu. Kuupata utepe huu kunahitaji kupiga malapa kwa ujuzi ndani ya maji kwa wakati maalum uliotengwa. Wale wasio na utepe huu hawawezi kuogelea katika sehemu yenye kina kirefu ya kidimbwi.
- Mbio za masafa marefu: lazima mbio za masafa marefu zifanyike kwa wanafunzi wa shule nzima katika muhula wa kwanza. Kwa kawaida nia za mbio hizo ni kuduru Eastleigh kupitia Mlango Kubwa hadi Pangani, kisha Kariokor na kisha kurejea Starehe -kisha kuoga kwa maji baridi shadidi na labda kuosha vyoo.
- Gwaride: ni lazima na kuwepo kwa kila mmoja kunahakikishwa bila kelele. Kiranja anatembea kwenye safu na kusikia wanafunzi wakizisema nambari zao kulingana na sajala la darasani. Namnbari isiyosemwa ina maana kwamba mwenye we hayupo. Wanafunzi wanapiga foleni ya gwaride kwa ajili ya kukaguliwa kwa njia ya kijeshi.
- Roll Call: ni kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wapo shuleni kulingana na mabweni kunakofanyika saa 12.00 jioni wakiwa wameketi kuzunguka uwanja wa jumuia. Wanafunzi wa vidato vya kwanza na pili hukaa chini (safi sana) nao wale wa kidato cha tatu na nne husimama. Majina ya mwisho huitwa. Waliotumiwa barua hupewa. Wanafunzi wa vidato vya tatu na nne kwa kawaida hupata barua zao wakati wa mapumziko ya asubuhi.
! Baada ya mashindanoya michezo, washindi huyakejeli mabweni shinde kwa kushangilia kwa sauti.
- Katika civilian(civile): nguo zisizo sare rasmi ya shule. Ni wanafunzi wa kidato cha tatu na nne tu wanaoweza kuondoka shuleni bila sare ya shule. Mwanafunzi wa kidato cha kwanza au cha pili anayepatikana katika nguo zisizo sare ya shule nje ya shule huwekwa kwenye "Patrol" (Tazama "Patrol" hapo juu)
- JIna la Faili/File Number: Ni kitambulisho cha mwanafunzi. Wakati wa kutoa adhabu, kiranja huuliza tu nambari ya faili ya mtuhumiwa. Mkosaji atahitaji kutazama "Bango la Matangazo" ili kuhakikisha kwamba "amefiksiwa" kwa ajili ya adhabu. Usipomkumbusha kiranja ambaye alikuahidi adhabu "kukufiksi" ni kosa kivyake na linaweza kuadhibiwa upya. Kuweka majina kwa ajili ya adhabu hufanyika katika Chumba cha Viranja. Kunao waliowekwa kwenye adhabu kwa "Kumtoroka Simba (tazama Simba/Lion" hapo juu) ilihali Simba hakuwa amewaambia kufanya chochote.
- Combiner/Mchanganyi: Mwanafunzi asiyetaka kula anaweza kukuambia umlie chakula, kwa utakuwa umechanganya milo ile miwili. Wanafunzi wanaokosa kuhudhuria milo bila ruhusa wanaweza kuambiwa kulipa fidia kwa ajili ya kuharibu chakula - ingawa "kimechanganywa".
- Kazi ya hiari: huhusisha huduma kwa jamii katika siku zote za likizo. Wanafunzi wa Starehe huipenda sana.
- Kukariri aya:
Ni adhabu nyingine kwa anayevunja masharti kuhusu lugha. Kwa madhumuni ya kielimu, wanafunzi wanatakiwa kuzungumza kwa Kiingereza kila siku ya wiki isipokuwa Jumapili. Hii ni kwa sababu masomo yote huwa katika Kiingereza na ni lazima kila mmoja ajizoeze lugha hiyo. Katika adhabu ya kukariri aya, mwadhibiwa hupewa shairi, mfano wa 'IF' poem la Rudyard Kipling. Mwadhibiwa atahitaji kulishika akilini na kulikariri kwa kiranja anayehusika na adhabu hii.
- Mazoezi ya nyimbo: hufanyika kila Alhamisi baada ya wakati wa mkutano wa jioni katika Ukumbi wa Mikutano. Wanafunzi huruhusiwa kuondoka tu baada ya wimbo huo kujulikana kikamilifu na kuweza kuimbika vizuri.
- Wakati wa Michezo: Wakati huu ni baina ya saa 10.30 na saa 12 jioni.Wanafunzi wote wa kidato cha kwanza na cha pili lazima waende kucheza kwenye uwanja ulio sehemu ya pili ya shule la sivyo wanaweza kuwekwa kwenye adhabu ya "Patrol". Wanafunzi wa kidato cha tatu na nne wanaweza kwenda maktabani. Wengine huelekea mjini.
- Mpiga picha: anayepiga picha shuleni kama bishara yake ya binafsi. Kamera bora huleta biashara bora pia.
- Mbuzi: mikutano ya kila mwezi ya waliokuwa wanafunzi wa Starehe inayofanyika hasa Parklands Sports Club mjini Nairobi; miongoni mwa maeneo mengine duniani.
- Gata: hiini mipira inayovaliwa kwenye soksi ili kuziwekelea ziwe juu, zikionyesha rangi za shule kwenye soksi hizo. Ni lazima kuvaliw ahata kama soksi ziko juu. Wanafunzi wa Starehe wanajulikana kama wanafunzi safi.
- Colours: tuzo la kutambuliwa katika michezo. Ni kama kupata Uteuzi Maalum kwa huduma shuleni katika nyanja fulani, kwa mfano pira wa magongo. Hutolewa rasmi katika Ukumbi wa Mikutano na kushonwa kwenye koti la mshindi na mshoni wa shule.
- Wajibu: kila mwanafunzi ana wajibu angalau mmoja katika eneo lolote kwa kipindi fulani. Kuwajibika ni jukumu la kila mwanafunzi wa Starehe. Kuwa mwanafunzi wa Starehe kwenyewe ni wajibu unaolindwa na kila mmoja.
- Ivory Tower: Ofisi ya Mkurugenzi. Ina sakafu ya mbao ngumu na makombe na ngao zimejaza mashubaka. Ni chumba chenye uluwa na utajiri wa nafasi yake.
- Jopo la Viranja Wakuu: linajumuisha Mkurugenzi pamoja na viranja wakuu wa shule, manaibu wao, Simba na Viranja wakuu wa mabweni. Mikutano jopo la viranja wakuu hufanyika siku ya Jumapili jioni baada ya chakula cha jioni.
- Uwanja wa Jumuia/Quad: Eneo lenye nyasi ambako ni viranja wakuu na walimu wanaweza kukanyaga. Hakuna ishara inayotoa amri hii lakini yeyote anayejifunza Starehe huishika amri hii kwa haraka sana. Wanabendi hutumbuiza kwenye uwanja huu kila Ijumaa na wanafunzi wengine wanaweza kukanyaga kwenye eneo hili baada ya "Ibada ya Mwisho ya Kuondoka"
- Ibada ya Mwisho ya Kuondoka: Hii ni ibada ya huzuni na mazingatio ambapo Mkurugenzi huwapa "Kiapo" wale wanaoondoka shuleni na kuwapa vyeti vyao vya Kuondoka shuleni.
- Kubrizi: Ni kukosa msichana wakati wa hafla shuleni au nje ya shule.
- Kufloti: Kutoweza kuelewa maelezo ya mwalimu darasani.
- Kugitch: Ni kuelewa.
- Ngebe/Gass: upuzi. Wakati mtu anasema kitu ambacho sni upuzi, anasemekana kwamba ametoa gass au ngebe.
- Mea: Kuwa mkomavu!. Mara nyingi huambiwa aliyesema jambo ambalo ni upuzi kwa wengine.
- Quarter Maji Mlo wa kipekee shuleni Starehe. Ni robo mkate na kabeji lililopikwa kupita kiasi na kujazwa maji. Wengine hukiita chakula hiki .25 Water
Shule ya Wavulana ya Starehe ilihitimisha miaka 50 mnamo mwaka 2009. Shule ya wasichana ilizinduliwa mnamo mwaka 2005. Katika mwaka huo wa Jubilei ya Dhahabu, Starehe ya Uingereza ilizindua mwito wa miaka miwili na nusu ili kujaribu kuruzuku mustakabali wa shule hizi mbili- wito unaoiotwa STarehFuture Appeal. Ufadhili unahitajika kujenga au kuboresha vifaa vya shule na kujenga Wakfu wa Griffin. Ruzuku hii inatarajiwa kuhakikisha kwamba kutakuwa na nafasi za bure katika shule zote mbili milele. Fedha zinazopatikana Uingereza zinatarajiwa kuongezea fedha zinazopatikana kwa kuchangisha nchini Kenya.