Susan Basemera ni mwimbaji na mwigizaji wa Uganda.
Basemera alianza kuimba kwenye kwaya za shule akiwa na miaka nane. Akifahamika kama Lady C nchini mwake, alipata mafanikio makubwa mwaka 1995, alipojiunga na bendi ya waka waka na kuachia nyimbo iliyojulikana "Yimilila awo".[1] alikuwa maarufu kwa wimbo "Ndoowa", uliokuwa wimbo bora mwaka [[1997]] na bado ni maarufu mpaka sasa. Mwaka [[2012]]
, Basemera alihamia Marekani kuendeleza Sanaa yake .[2] Japo akijikita Zaidi katika uigizaji, aliachia nyimbo "Goolo Goolo" mnamo [[2015]].[3]
Mwaka 2016, Basemera alitokea kwenye filamu fupi Gubagudeko akiwa na Mahershala Ali. Ameigiza kama muigizaji mkuu kwenye Can ''You Keep a Secret. Mwaka [[2020]],
Basemera ameigiza kama Yuliana kwenye tamthiliya ya Apple TV+ Little America |Little America, ikihusiana na hadithi za wahamiaji kwenda Marekani. Alipata nafasi hiyo baada ya muongozaji kutuma kipeperushi naye akatuma barua pepe kwenye anuani iliyokuwepo katika kipeperushi kile, na kuwafurahisha waandaaji katika onyesho la kuonyesha uwezo..[2] kwenye onyesho moja , akionyesha utamaduni wake kwa kuvaa a gomesi.[4]
Kulingana na Basemera, tasnia ya filamu ya Uganda ipo nyuma ya tasnia ya filamu ya Marekani kwa uzalishaji, vifaa, waigizaji na usambazaji. "Tasnia ikiwezeshwa na watu wazoefu inaweza kufanikiwa zaidi," alisema Basemera .[5]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)