Takalsitoli (kwa Kiingereza: Tacalcitol), inayouzwa kwa majina ya chapa Curatoderm na mengine, ni dawa inayotumika kutibu makovu makavu yanayowasha (psoriasis), haswa kovu la tauni.[1][2] Dawa hii inatumika juu ya ngozi mara moja hadi mbili kwa siku.[1][3]
Madhara yake yanaweza kujumuisha upele wa ngozi na kalsiamu nyingi.[1] Ni analogi ya vitamini <sub id="mwHw">D3</sub> inayotengenezwa.[3]
Takalsitoli iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Japani mwaka wa 1993.[4] Iko kwenye Orodha ya Shirika la Afya Ulimwenguni ya Dawa Muhimu kama njia mbadala ya kalsipotriolo (calcipotriol).[5] Nchini Uingereza, gramu 30 hugharimu Huduma ya kitaifa ya Afya (NHS) takriban £13 kufikia mwaka wa 2023.[6]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)