The Tech | |
---|---|
Jina la gazeti | The Tech |
Aina ya gazeti | Gazeti la Wanafunzi wa Chuo Kikuu |
Lilianzishwa | 16 Novemba 1881 Kwenye mtandao : 1993 |
Eneo la kuchapishwa | Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts Maarufu kama: MIT |
Nchi | |
Mwanzilishi | Arthur W. Walker |
Mchapishaji | Charles River Publishing (2000-2009) Saltus Press |
Makao Makuu ya kampuni | Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts |
Tovuti | http://tech.mit.edu/ |
The Tech, lililochapishwa kwa mara ya kwanza 16 Novemba 1881, ni gazeti kongwe kabisa na kubwa kabisa la kampasi katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (Massachusetts Institute of Technology-MIT). Linapatikana katika eneo la Cambridge, Massachusetts. Matoleo huchapishwa Jumanne na Ijumaa katika mwaka wa masomo, kila siku katika kipindi cha wanafunzi wapya kuripoti, mara moja kwa wiki katika mwezi wa Januari na mara kadhaa katika majira ya joto. Nakala huchapishwa na husambazwa kote katika kampasi ya MIT katika asubuhi hiyo ya uchapishaji.
The Tech ndilo gazeti la kwanza kuchapishwa kwenye mtandao wa tarakilishi za ulimwengu. Katika ukurasa mmoja wa tovuti yake kumeandikwa "Gazeti la kwanza la dunia kwenye mtandao ,lilianzishwa mwaka wa 1993." Hapo awali, StarText , mfumo wa aina ya videotex ya Fort Worth Star- Telegrams wa kuonyesha makala ya magazeti kwenye skrini za kompyuta, ilianzishwa katika mwaka wa 1982 katika Fort Worth, Texas. Ingawaje, mfumo wa StarText haukutumika kwenye mtandao mpaka mwaka wa 1996.Katika mwaka wa 1987, gazeti la Middlesex News (Framingham, Massachusetts) ilianzisha Fred Kompyuta, mfumo wa BBS uliotumika kuangalia toleo la siku inayofuata na ,hapo baadaye, mfumo huu ulitumika kuandaa makala ya filamu ya gazeti hili.
Karibu kila toleo la Tech hupatikana kwenye tovuti na matoleo mengi hupatikana kama faili za PDF. Kwa mfano, toleo la kwanza lililochapishwa: The Tech (16 Novemba 1881).[1] Lilihaririwa na Arthur W. Walker, kisha likachapishwa na Alfred Mudge & Son, Printers, wanaopatikana katika barabara ya 34 School Street katika Boston. Hivi sasa, gazeti la Tech linachapishwa na kampuni ya uchapishaji Mass Web Printing Company, kitengo cha Kundi la Phoenix Media/Communications Group linalochapisha Boston Phoenix. Kutoka mwaka wa 2000 - 2009, Tech lilichapishwa na Charles River Publishing katika Charlestown na ,kwa muda mfupi, Saltus Press katika Worcester, baada ya Saltus kununua CRP.
Kumbukumbu za The Tech zinapatikana katika tovuti yao.[2]