Them Mushrooms ni kundi la wanamuziki kutoka nchini Kenya lililobadilika baadaye na jina lao kuwa "Uyoga"[1].
Mitindo yao hasani Chakacha, Benga pamoja na reggae. Kundi hili lilianzishwa mwaka wa 1972 na ndugu watano Teddy Kalanda Harrison, Billy Sarro Harrison, George Zirro Harrison, John Katana Harrison na Dennis Kalume Harrison. Waliobaki hadi leo ni Billy Sarro na John Katana walioungwa na wanamuziki wengine.[2]
Walikuwa maarufu kimaitaifa kwa wimbo wao Jambo Bwana (1980) uliorudiwa na kurekodiwa na waimbaji wengi Kenya, Tanzania hadi Ulaya ambako Boney M. waliutoa pia. Kwa jumla nakala zinazozidi 200,000 za huo wimbo ziliuzwa.
Walianza kuimba kwenye hoteli za kitalii za Mombasa na pwani ya Kenya na mwaka wa 1987 walihamia Nairobi.[3]
Mwaka wa 2000 walipata tuzo la 'M-NET 2000 AWARD' linalotolewa na kituo cha TV cha Afrika Kusini M-NET Television Channel.
Them Mushroom walitoa albamu kadhaa.[4]:
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Them Mushrooms kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |