Todd Smith

Todd Smith
Todd Smith Cover
Studio album ya LL Cool J
Imetolewa 11 Aprili 2006
Imerekodiwa 2005-2006
Aina Hip hop
Urefu 51:47
Lebo Def Jam
Mtayarishaji Trackmasters
Tahakiki za kitaalamu
Wendo wa albamu za LL Cool J
The DEFinition
(2004)
Todd Smith
(2006)
Exit 13
(2008)
Single za kutoka katika albamu ya Todd Smith
  1. "It's LL And Santana / What You Want"
    Imetolewa: 10 Januari 2006
  2. "Control Myself"
    Imetolewa: 1 Februari 2006
  3. "Freeze"
    Imetolewa: 2006


Todd Smith ni albamu ya 11 (ya 12 kwa ujumla) ya rapa wa Kimarekani LL Cool J. Albamu ilitolewa mnamo tar. 11 Aprili 2006. Inamjulisha ushirikiano wake na baadhi ya wasanii kama vile Jennifer Lopez, Pharrell, Juelz Santana, Teairra Mari, Ginuwine, Mary J. Blige, 112, Mary Mary, Ryan Toby (kutoka City High) na Freeway.

Maelezo ya albamu

[hariri | hariri chanzo]

Single ya kwanza ni "Control Myself", ambayo imetayarishwa na Jermaine Dupri, ambayo pia ni ushirikiano wake mwingine na mwimbaji Jennifer Lopez baada ya ile ya kwanza ya "All I Have" kwenye albamu ya Lopez ya 2002, This Is Me... Then. LL Cool J na Jennifer Lopez walipiga video ya "Control Myself" mnamo tar. 2 Januari 2006 katika studio za Sony, New York. Video ilipigwa na Hype Williams. Awali, wimbo ilibidi ashirikishwe Fergie (kutoka katika kundi la The Black Eyed Peas), hata hivyo makubaliano ya kimalipo yameleta shida na kupelekea nafasi yake kuchukuliwa na Jennifer Lopez. Todd Smith imepata tahakiki za ajabu, japokuwa watathmini wengi walifurahishwa sana na kibao cha "Preserve The Sexy" na "Freeze". Freeze kilikuwa kibao cha pili kutoka katika albamu na kimemshirikisha msanii kama Lyfe Jennings. Albamu ilipeleka nakala 500,000 nchi za nje, lakini imeuza nakala 367,000 katika hizo.

Waliotayarisha albamu hii ni pamoja na Pharrell, Scott Storch, Bink, Shea Taylor, Keezo Kane na Trackmasters.

Albamu iliingia kwenye chati za Billboard #6, na kuuza kopi 116,000 na kushika nafasi ya #79 kwenye chati za albamu za UK na nafasi ya #40 nchini Kanada.[1]

Albamu imetunukiwa Dhahabu na RIAA.[2]

Orodha ya nyimbo

[hariri | hariri chanzo]
  1. "It's LL And Santana" (akimshirikisha Juelz Santana) (Imetayarishwa na Shea Taylor)
  2. "Control Myself" (akimshirikisha Jennifer Lopez) (Imetayarishwa na Jermaine Dupri)
  3. "Favorite Flavor" (akimshirikisha Mary J. Blige) (Imetayarishwa na Trackmasters)
  4. "Freeze" (akimshirikisha Lyfe Jennings) (Imetayarishwa na LL Cool J)
  5. "Best Dress" (akimshirikisha Jamie Foxx) (Imetayarishwa na The Neptunes)
  6. "Preserve the Sexy" (akimshirikisha Teairra Mari) (Imetayarishwa na Keezo Kane)
  7. "What You Want" (akimshirikisha Freeway) (Imetayarishwa na The Narcotics)
  8. "I've Changed" (akimshirikisha Ryan Toby) (Imetayarishwa na Trackmasters)
  9. "Ooh Wee" (akimshirikisha Ginuwine) (Imetayarishwa na Scott Storch)
  10. "#1 Fan" (Imetayarishwa na Trackmasters)
  11. "Down the Aisle" (akimshirikisha 112) (Imetayarishwa na Trackmasters)
  12. "We're Gonna Make It" (akimshirikisha Mary Mary) (Imetayarishwa na Bink)
  13. "So Sick (Remix)" (Ne-Yo akimshirikisha LL Cool J) (Imetayarishwa na Trackmasters) (US Bonus track)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Todd Smith kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.