Alopecia | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Infectious diseases |
ICD-10 | L65.9 |
ICD-9 | 704.0 |
DiseasesDB | 14765 |
MeSH | D000505 |
Upara (kwa Kiingereza baldness) ni hali ya kutokuwa na nywele au ukosefu wa nywele mahali ambapo mara nyingi hukua, hasa kichwani. Aina ya upara ya kawaida zaidi ni upungufu wa nywele unaowatokea hatua kwa hatua binadamu wanaume na viumbehai wengine na ambayo huitwa "mkondo wa upara wa kiume".
Kiasi na mikondo ya upara vinaweza kutofautiana sana, baina ya mikondo ya kiume na ya kike ya alopeshia (androgenic alopecia au alopecia androgenetica), alopecia areata, ambayo huhusisha upotevu wa baadhi ya nywele kichwani na alopecia totalis, ambayo huhusisha upotevu wa nywele zote kichwani, hadi aina iliyokithiri zaidi ambayo ni universalis alopecia, inayohusisha kupoteza nywele zote kichwani na mwilini.
Istilahi alopeshia hutokana na neno la Kigiriki αλώπηξ, alópex, inayomaanisha mbweha. Asili ya matumizi hayo ni kuwa mnyama huyu huvua manyoya yake mara mbili kwa mwaka.
Ishara ya upara ni ukosefu wa nywele juu ya kichwa cha mtu.
Matukio ya upara wa kiolezo hutofautiana miongoni mwa idadi kubwa ya watu kwa misingi ya maumbile ya jeni; sababu za kimazingira hazionekani kuathiri sana aina hii ya upara. Utafiti mmoja mkubwa uliofanywa katika Maryborough, Victoria, Australia ulionyesha kuwa kiwango cha ya upotezaji nywele za mbeleni mwa kichwa-katikati hulingana na ongezeko la umri na huathiri 73.5% ya wanaume na 57% ya wanawake wenye umri wa miaka 80 na zaidi. Kwa mujibu wa tovuti ya Medem Medical Library, upara wa kiume huathiri takribani wanaume milioni 4 nchini Marekani. Takriban asilimia 25 ya wanaume huanza kupata upara tokea umri wa miaka 20, theluthi mbili huanza kupata upara kuanzia miaka 60. Uwezekano wa kupata jeni ya upara ni 4 kwa 7.
Mkondo wa wanaume hudhihirisha upungufu wa nywele kutoka pande za paji la kichwa unaojulikana kama "upeo wa nywele unaopungua". Upungufu wa upeo wa nywele huonekana katika wanaume waliozidi miaka 20 lakini unaweza kuonekana mapema, mwishoni mwa umri wa ujana pia.
Sehemu ndogo ya upara inaweza kujitokeza sehemu ya juu (vertex). Sababu za aina hii ya upara (uitwao androjenetic alopecia) ni DHT, homoni yenye msukumo wa nguvu za ngono, ukuaji wa nywele za mwilini na usoni, ambayo huweza kuathiri vibaya tezi kibofu pamoja na nywele za kichwani.[1]
Bado haijafahamika kikamilifu namna ambayo DHT hutekeleza jambo hili. Kwenye ngozi za vichwa zinazoathirika na jeni hii, DHT huzua mchakato wa ukondefu wa nywele. Kupitia mchakato wa ukondefu wa nywele, upana wa mzizi wa nywele huendelea kupungua kitaratibu hadi nywele kwenye ngozi ya kichwa kufanana na manyoya hafifu au "sufi za pichi" au hata kutoweka kabisa. Mwanzo wa kupoteza nywele wakati mwingine huanza mapema mwishoni mwa ubalehe na hasa husababishwa na jeni. Upara wa mkondo wa kiume huainishwa katika kipimo cha Hamilton Norwood I-VII.
Iliaminika awali kuwa upara ulirithiwa kutoka kwa babu wa ukoo wa mama. Ingawa pana misingi ya imani hii, wazazi wote huchangia uwezekano wa vizalia wao kupoteza nywele. Pana uwezekano mkubwa zaidi wa kurithi upara iwapo mchanganyiko wa jeni zinazosheheni kwa nguvu kutoka wazazi wote zina hali hiyo.
Kuna aina nyingine nyingi za upara:
Hakuna makubaliano kuhusu maelezo ya mageuzi ya mkondo wa upara wa kiume. Madai ya kwamba mkondo wa upara wa kiume (MPB) hunuiwa kuwasilisha ujumbe wa kijamii unaungwa mkono na ukweli kwamba msambao wa vihisivu androjeni kwenye ngozi ya kichwani hutofautiana baina ya wanaume na wanawake, aidha waume na wake wazee walio na viwango vya juu vya androjeni mara nyingi hudhihirisha ukondefu wa nywele uliotawanyika, kinyume na ilivyo katika mkondo wa upara wa kiume.
Nadharia moja, iliyotolewa na Muscarella na Cunningham,[6] inaeleza kuwa upara ulijitokeza miongoni mwa wanaume kufuatia uteuzi wa jinsia kama ishara pevu ya uzee na ukomavu wa kijamii, ambapo uchokozi na tabia za kujihatarisha huongezeka. Hii ilitoa taswira ya mwanamume aliyefikia hali iliyoimarika kijamii lakini aliyepungukiwa na uwezo wa kimwili wa kupata washirika wa kujamiiana na kukuza watoto hadi utu uzima.
Katika utafiti wa Muscarella na Cunningham[6] , wanaume na wanawake walitazama wanamitindo 6 wa kiume waliokuwa na viwango tofauti vya nywele usoni (walio na ndevu na masharubu au bila) na nywele kichwani (kichwa kilichojaa nywele, zinazopungua na upara). Washiriki walitathmini kila mafungu kwa kutumia vivumishi 32 vilivyohusiana na mitazamo ya jamii. Wanaume waliokuwa na upara ama waliokuwa na nywele usoni au nywele zinazopungua walichukuliwa kuwa wenye umri mkubwa zaidi kuliko wale ambao waliokuwa wamenyolewa kabisa au waliokuwa na nywele nyingi kichwani. Ndevu na kichwa kilochojaa nywele zilionekana kama hali ya ujasiri zaidi na kutokomaa kijamii, nao upara ukahusishwa na ukomavu zaidi kijamii. Hariri ya maoni ya kijamii kuhusu mikondo ya upara wa kiume umetolewa na Henss (2001).[7]
Nadharia tete nyingine za mageuko ya kimaumbile ni pamoja na miunganiko baina ya jeni kwa sifa bainishi zenye manufaa zisizohusiana na nywele wala utofauti wa jeni.
Upara si tu ni sifa bainishi ya binadamu. Viumbe wengine wa jamii ya nyani, kama vile masokwe, makakiu wenye mikia minene, na uakari wa Amerika ya Kusini hudhihirisha ukondefu taratibu wa nywele kichwani baada ya kubalehe. Makakiu wazima wenye mikia minene, kwa kweli, hutumika mara nyingi maabarani katika kutafiti matibabu yasaidiayo ukuaji wa nywele.
Watangulizi mbalimbali wa tai wa Ulimwengu wa Kale na Ulimwengu Mpya waligeuka kwa kipindi cha wakati na kupata upara kichwani, iliyozuia manyoya kushika vipande vya nyama zilizooza kutoka mlo wa tai, na kusaidia pia kupunguza joto.[8]
Utafiti mwingi ulifanywa kuhusu maumbile ya jeni zinazohusiana na mkondo wa upara wa kiume, au androgenetic alopecia (AGA). Utafiti unaonyesha kwamba kwa kiasi kikubwa, uwezekano wa kupatwa na upara wa mapema wa kiume hutokana na jeni za chembeuzi X. Jeni nyingine zisizohusiana na ngono pia hushirikishwa.
Watafiti wa Ujerumani wanataja jeni pokezi ya androjeni kama kiungo muhimu zaidi cha upara.[9] Wanahitimisha kwamba aina fulani ya jeni pokezi ya androjeni huhitajika kwa ukuaji wa AGA. Mwaka huohuo matokeo ya utafiti huu yalithibitishwa na watafiti wengine.[10] Jeni hii ni dhaifu, kwa hivyo mwanamke huhitaji kromosomu mbili za X zenye kasoro ili kuonyesha alopeshia ya mkondo sawa na wa kiume. Kwa vile androjeni na mahusiano yake na kipokezi cha androjeni ndiyo sababu za AGA inaonekana jambo la kimantiki kuchukulia kuwa jeni hisivu ya androjeni ina jukumu muhimu katika ukuaji wake.
Utafiti mwingine wa mwaka 2007 ulipendekeza kuwa jeni nyingine katika kromosomu X, iliyo karibu na jeni pokezi ya androjeni, ilikuwa na jukumu muhimu katika mkondo wa upara wa kiume. Walipata kuwa eneo la Xq11-q 12 katika kromosomu X- lilihusiana pakubwa na AGA katika wanaume. Walisisitiza kuwa EDA2R ndiyo jeni inyohusiana zaidi na AGA. Utafiti huu umeigwa katika angalau tafiti tatu huru zifuatazo.
Jeni nyinginezo zinazohusika na upotevu wa nywele zimegunduliwa. Mojawapo ikiwa jeni ya kromosomu 3. Jeni huwa iko katika 3q26.[11] Jeni hii pia huchangia katika aina ya upara unaohusishwa na ulemavu wa akili. Jeni hii ni dhaifu.
Jeni nyingine ambayo inaweza kushiriki katika upotevu wa nywele ni P2RY5. Jeni hii inahusika na muundo wa nywele. Baadhi zinaweza kusababisha upara wakati wa kuzaliwa ilhali aina nyinginezo husababisha "nywele za sufu".[12]
Utafiti wa hivi karibuni ulithibitisha jeni pokezi X zinazohusiana na androjeni kuwa za muhimu zaidi. Huku jeni katika kromosomu 20 ikiwa ya pili kwa umuhimu wa kuchangia hali hiyo (snpedia)
Ingawa upara si kawaida sana katika wanawake kama ilivyo kwa wanaume, athari za kisaikolojia za kupoteza nywele huwa kubwa zaidi. Kwa kawaida ukanda wa nywele za mbele hudumu ilhali uwingi wa nywele hupungua katika maeneo yote kichwani. Hapo awali iliaminika kuwa ilisababishwa na testosteroni sawa na katika upara wa kiume, lakini wanawake wengi ambao kupoteza nywele huwa na viwango vya kawaida vya testosteroni.
Hata hivyo, upotezaji nywele kwa mwanamke umekuwa tatizo linaloendelea, ambalo kwa mujibu wa Akademia ya Marekani ya Matibabu ya ngozi, huathiri karibu wanawake 30,000,000nchini Marekani. Ingawa upotezaji nywele kwa wanawake kwa kawaida hutokea baada ya umri wa miaka 50 au hata baadaye, isipoambatana na matukio kama ujauzito, maradhi sugu, ya mlo, na mfadhaiko kati ya nyinginezo, kwa sasa inatokea miaka ya mapema na huku ripoti zikionyesha kuwa hutokea hata wanawake wachanga kama wa miaka 15 au 16.[13]
Sababu za upotevu wa nywele mingoni mwa wanawake zinaweza kutofautiana na zinazoathiri wanaume. Kuhusiana na alopeshia androjeni, upotevu wa nywele za wanawake hutokea kulingana na athari za homoni za androjeni (testosteroni, androsteinedioni, na dihaidrotestosteroni (DHT)). Homoni hizi za kiume, kwa kawaida hutokea kwa kiasi kidogo kwa wanawake.
Hata hivyo, kulingana na Ted Daly, MD, tabibu wa ngozi kutoka Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Long Island, alopeshia androjeni sio sababu kuu ya kupotea kwa nywele kwa wanawake na wataalamu wa ngozi kwa sasa hupendelea kuita hali hii mkondo wa upotevu wa nywele kwa wanawake badala ya kutumia neno androjeni alopeshia. Anaongeza kuwa mkondo wa kike ni wa mtawanyiko na hudhihirika katika eneo lote la juu ya kichwa na waweza kuathiri wanawake wakati wowote.[14]
Wakati mwingine pia mchakato wa homoni huweza kusababisha upotevu wa nywele kwa mwanamke. Baadhi ya mifano ni: uja uzito, kufikia kutoweza kuzaa, uwepo wa uvimbe wa ovari, dawa za kudhibiti upataji mimba na kiwango juu cha androjeni, dalili za vimbe nyingi za ovari. Pia matatizo ya tezi, anemia, ugonjwa sugu na baadhi ya dawa husababisha upotevu wa nywele kwa mwanamke .[15]
Alopeshia kutokana na kemotherapi ya saratani imeripotiwa kusababisha mabadiliko katika dhana-nafsia na taswira ya mwili. Taswira ya mwili hairejelei hali ya awali baada ya kuota upya kwa nywele kwa idadi kubwa ya wagonjwa. Katika hali kama hizo, wagonjwa hutatizika kuonyesha hisia zao (alexithymia) na hutaka zaidi kujiepusha na migogoro ya familia. Tiba ya familia inaweza kusaidia familia kukabiliana na matatizo ya kisaikolojia yakijitokeza.[16]
Matatizo ya kisaikolojia kutokana na upara, yakiwepo, kwa kawaida hushamiri zaidi mwanzoni mwa dalili.[17]
Baadhi ya wanaume wenye upara huonea fahari upara wao, wakihisi unasaba na watu maarufu wenye haiba walio na upara kama vile Yul Brynner, Bruce Willis, Vin Diesel, Sean Connery, Jason Statham, Patrick Stewart, Ben Kingsley, "Stone Cold Steve Austin, Tupac Shakur, Michael Chiklis , Telly Savalas, na Jeffrey Eugenides. Larry David hasa hutumia upara wake kama njia ya ucheshi-nafsia katika vipindi vyake vya televisheni vya Seinfeld and Curb Your Enthusiasm. Katika miaka ya hivi karibuni, upara ,umekuwa si tatizo kubwa kutokana na ongezeko la mtindo wa kudumisha nywele fupi sana, au hata kunyoa nywele kabisa, miongoni mwa wanaume katika nchi za magharibi. Kwa mfano, Patrick Stewart alitajwa kama "Mume wa Kuvutia zaidi kwenye TV" kwa jukumu lake la haiba kama Kapteni Jean-Luc Picard.
Makampuni mengi yamefanikiwa kibiashara kwa kuuza bidhaa ambazo hugeuza hali ya upara, kwa ukuzaji nywele upya, upandikizaji nywele kwa upasuaji au kuuza vibandiko vya nywele.
Matibabu ya aina mbalimbali za alopeshia huwa na mafanikio madogo. Baadhi ya waliopoteza nywele hutumia matibabu yaliyothibitika kiafya kama vile finasteridi, dutasteridi na mchanganyiko wa minoksidili inayotumiwa katika jaribio la kuzuia upotevu zaidi ya nywele na kuikuza upya. Kama kanuni ya jumla, ni rahisi kudumisha nywele zilizosalia kuliko kukuza upya, hata hivyo, matibabu yaliyotajwa yanaweza kuzuia kupotea kwa nywele kutokana na Androjeni alopeshia , na kuna teknolojia mpya katika upasuaji wa kujirembesha wa kupandikiza na mifumo ya uwekaji nywele ambayo huenda yasitambulike kabisa.
Nchini Marekani pana tiba aina mbili za dawa, ambazo zimeidhinishwa naShirika la Usimamizi wa Chakula na Dawa la Marekani (FDA) ikiwemo bidhaa moja iliyokubaliwa na FDA kwa matibabu ya alopeshia androgeni, inayojulikana pia kama mkondo wa kupoteza nywele wa kiume au wa kike. Matibabu mawili yaliyoidhinishwa na FDA ni finasteridi (inayotangazwa kama propeshia kwa kutibu upotevu wa nywele) na minoksidili.
Uchunguzi unaonyesha kupungua kwa testosteroni bure pamoja na kuongezeka kwa nguvu kutokana na mafunzo(yasiyobainika)ya utaratibu wa nguvu.
Kupunguza mfadhaiko kunaweza kusaidia kupunguza kasi ya upotevu wa nywele.
Vizuiakinga-mwili vinavyotumiwa kichwani zimeonyeshwa kugeuza kwa muda alopeshia areata, ingawa madhara ya baadhi ya dawa hizi husababisha maswala kuzushwa kuhusu dawa hizi.[18][19]
Njia moja ya kuficha upotevu wa nywele ni mtindo wa kuchana "kufunika", ambapo nywele zilizosalia hutengenezwa kwa mkao wa kufidia eneo la upara. Hii aghalabu huwa suluhisho la muda, na hufidia tu iwapo eneo lililipoteza nywele ni ndogo. Jinsi upotevu wa nywele huongezeka , kuchana "kufunika" hauweza tena kutegemewa. Wakati hali hii hufikia hatua ya juhudi kubwa na manufaa madogo-inaweza kumfanya mtu kukejeliwa au kudharauliwa.
Njia nyingine ni ya kuvaa kofia au kibandiko cha nywele- wigi au nywele za bandia. Wigi ni safu ya nywele bandia au halisi ambazo kwa kawaida hutengezwa kwa mitindo inayofanana na nywele za kawaida. Mara nyingi nywele hizi ni bandia. Wigi hutofautiana sana katika ubora na gharama. Nchini Marekani, wigi bora zaidi-ni zile zinazofanana na nywele halisi-hugharimu hadi kumi ya maelfu ya dola. Mashirika pia hukusanya 'michango ya nywele asili za watu binafsi ili kutengenezea wigi kwa wagonjwa wachanga wa saratani yaambao wamepoteza nywele zao kutokana na kemotherapia au matibabu mengine ya kansa mbali na aina yoyote ya upotevu wa nywele.
Ikumbukwe kuwa idadi kadhaa ya vibandiko maarurufu mbadala vipo kama vile Nanogen (Uropa) na Toppik (Marekani) nazo ni maarufu sana kama vipodozi visivyo vya wigi ambavyo huchangia unyuzi-embamba wa elektrostati kwa nywele za mtu binafsi.
Ingawa si kawaida kama vile upotevu wa nywele kichwani, kemotherapia, kutosawazika kwa homoni, aina za alopeshia, na sababu nyinginezo zinaweza pia kusababisha upotevu wa nywele katika nyusi. Nyusi bandia hupatikana kufidia nyusi zisizokuwepo au kufunika nyusi zenye mianya. Uchoraji mdogo sana wa kuchanja pia huwezekana.
Badala ya kuficha upotevu wa nywele, mtu anaweza kuikubali hali hiyo. Kichwa kilichonyolewa huotesha vishina kwa namna na kiwango sawa na unyoaji wa nywele za usoni. Umma kwa jumla umeweza kukubali unyoaji wa kichwa pia, lakini upara wa wanawake bado haujakubalika sana kijamii.
Pana visasili vingi kuhusiana na sababu za upara na ulingano wazo na nguvu za kiumeza mtu, uwerevu wake, kabila, kazi, tabaka la kijamii, utajiri n.k. Ingawa kutia shaka kunatarajiwa kutokana na ukosefu wa ithibati za kisayansi, baadhi ya visasili hivi vina kiwango cha ukweli wa kimsingi .
Utafiti unaangazia uhusiano kati ya upotevu wa nywele na masuala mengine ya afya. Ingawa pamekuwepo uvumi juu ya uhusiano kati ya kuanza mapema kwa-androjeni alopeshia na maradhi ya moyo, upitiaji upya wa makala kuanzia 1954-1999 haikupata uhusiano wa kudumu kati ya upara na ugonjwa wa mishipa ya moyo. Wataalamu wa ngozi walioendesha shughuli hiyo walipendekeza utafiti zaidi unahitajika.
Sababu za kimazingira zinachunguzwa upya. Utafiti wa mwaka 2007 ulionyesha kuwa uvutaji sigara unaweza kuwa sababu inayohusishwa na upotevu wa nywele kutokana na uzee miongoni mwa wanaume wa Kiesia. Utafiti huu uliozingatia maswala ya umri na historia ya familia, ulipa takwimu kubwa ya uhusiano chanya kati ya androjeni alopeshia kali au wastani na uvutaji sigara.[28]
Katika Mei 2007, watafiti katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania walivumbua njia mpya ya kisayansi ambayo huenda ikatibu upara kwa seli shina. Bidhaa hii inaweza kuwa sokoni katika muda wa miaka mitatu ijayo.[29][30] Watafiti waligundua kwamba ukuaji wa shina mpya zinazoweza kuotesha nywele uliweza kusisimuliwa katika panya kwa kuharibu ngozi zao.[31]
Februari 2008 watafiti katika Chuo Kikuu cha Bonn walitangaza kugundua msingi wa kijentiki wa aina mbili tofauti ya ipotevu wa nywele uliorithiwa, hivyo basi wakafungua njia pana ya matibabu ya upara. Ukweli kwamba kipokezi mahususi kilikuwa na wajibu maalum katika ukuaji wa nywele haukujulikana awali kwa wanasayansi na kutikana na maarifa haya mapya, tafiti zinazolenga kugundua jeni zaidi za aina hii huenda ikachangia ongezeko la tiba kwa aina tofauti za upotezavu wa nywele.[32][33]
Utafiti wa miezi minane katika Taasisi ya Sayansi ya Dawa katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Malaysia ulionyesha virutubisho vya kila siku vilivyodhihirishwa vya tokotrienoli(vitamini E) tata inaweza kuongeza ukuaji wa nywele kwa watu wenye mkondo wa upara wa kiume kwa asilimia 42.[34]
Mnamo Mei 2009, watafiti kule Ujapani walitambua jeni, SOX21, inayoonekana kuwa ndiyo yenye wajibu wa upotevu wa nywele kwa watu.[35]
{{cite journal}}
: Unknown parameter |month=
ignored (help)
{{cite web}}
: Unknown parameter |dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: Unknown parameter |month=
ignored (help)
{{cite web}}
: Unknown parameter |dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: Unknown parameter |month=
ignored (help)
{{cite journal}}
: Explicit use of et al. in: |author=
(help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: Explicit use of et al. in: |author=
(help); Unknown parameter |month=
ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite journal}}
: Unknown parameter |month=
ignored (help)
{{cite web}}
: Unknown parameter |=
ignored (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20081219094737/http://video.msn.com/?mkt=
ignored (help)
Wikisource has the text of the 1911 Encyclopædia Britannica article Upara. |
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)