Vivutio vikuu vya watalii vya Botswana ni mapori ya akiba, pamoja na uwindaji na safari za kupiga picha. Vivutio vingine ni pamoja na eneo la Delta ya Okavango [1], ambalo wakati wa mvua maji upita, visiwa na maziwa. [2] Sekta ya utalii pia ilisaidia kuleta ukuaji wa uchumi wa Botswana kutoka vyanzo vya jadi kama vile almasi na nyama ya ng'ombe na kutoa nafasi za kazi 23,000 mwaka wa 2005. [3]
Mwaka wa 1999, kulikuwa na vyumba 2,100 vya hoteli na vitanda 3,720 na kiwango cha 53% cha watu wanaokaa. Wageni 843,314 waliwasili Botswana mwaka huo na zaidi ya 720,000 kutoka nchi nyingine za Afrika. Mapato ya utalii katika mwaka wa 2000 yalifikia dola milioni 313. Mwaka 2003, Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilikadiria wastani wa gharama ya kila siku ya kukaa Gaborone kuwa $129, ikilinganishwa na Kasane ya $125. Gharama iliweza kushuka chini hadi $50 katika maeneo mengine ya nchi. [4] Botswana inachukuliwa kuwa nchi salama zaidi kutembelea barani Afrika. [5]
Wageni wengi waliofika Botswana wakati wa likizo zao walitoka nchi zifuatazo : [6]
Nchi | 2016 | 2015 | 2014 | 2013 |
---|---|---|---|---|
Zimbabwe | 874,169 | 967,322 | 784,720 | 825,717 |
South Africa | 759,564 | 808,118 | 600,387 | 742,639 |
Zambia | 220,649 | 202,289 | 188,351 | 331,799 |
Namibia | 187,044 | 170,326 | 162,453 | 169,733 |
United States | 52,171 | 49,451 | 49,961 | 139,752 |
United Kingdom | 42,534 | 41,011 | 39,675 | 47,929 |
Germany | 35,288 | 32,230 | 34,576 | 43,674 |
India | 19,297 | 17,413 | 18,342 | 13,543 |
Lesotho | 18,773 | 18,842 | 12,408 | 10,839 |
Malawi | 17,102 | 20,607 | 15,175 | 17,386 |
Total | 2,401,786 | 2,501,616 | 2,082,521 | 2,598,158 |
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |