Uwanja wa michezo wa Nakivubo

Uwanja wa michezo wa kumbukumbu ya Vita vya Nakivubo


Uwanja wa michezo wa kumbukumbu ya Vita vya Nakivubo ambao hujulikana kama Uwanja wa Nakivubo ni uwanja wenye malengo mengi huko Kampala nchini Uganda. Hivi sasa haitumiki lakini hapo awali ulitumika zaidi kwa mechi za mpira wa miguu na pia ulitumika kama ukumbi wa nyumbani wa klabu ya SC Villa. Uwanja huo ulikuwa na uwezo wa kuchukua idadi ya watu 30,000, baada ya ukarabati wa mwaka 2013, lakini kabla ya ukarabati unaoendelea wa mwaka 2017.[1] Unatarajiwa kuwa na uwezo wa watu 35,000 baada ya kukamilisha kwa kazi zinazoendelea.[2]

Uwanja huo upo Wilaya ya Kati ya Biashara ya Jiji la Kampala Umezungukwa naUwanja wa Ununuzi wa Ham',[3] ndani ya umbali wa kutembea kutoka Hifadhi mpya ya Teksi.[4]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Uwanja huu ulianzishwa mwanzoni mwa mwaka 1926,[5] uliboreshwa na kufanywa wa kisasa mnamo mwaka 1954 na serikali ya kikoloni ya britain kuadhimisha maisha ya Waganda waliouawa wakati wa Vita vya dunia vya pili kufuatia kupitishwa kwa "Sheria ya Kumbukumbu ya Vita vya Nakivubo" na Bunge la Uganda.[6]

Mnamo mwaka 2000, uwanja huu ulitumika kuaandaa mechi ya timu ya kitaifa ya mpira wa miguu ya Uganda na wachezaji wote wakiwa wamevaa jezi za FC Internazionale Milano.[7] Walipigwa faini kwa hiyo.


Muhtasari

[hariri | hariri chanzo]

Uwanja wa Nakivubo ulibuniwa mnamo mwaka 1926 kwenye ardhi iliyotolewa na Kabaka ya Buganda wakati huo.[5] ulitumika kuandaa mechi yake ya kwanza mnamo 1 Aprili mwaka 1926 kati ya Timu ya Kitaifa ya Uganda na Timu ya Kitaifa ya vijana chini ya miaka 18 ya Uganda.[8] unamilikiwa na Serikali ya Uganda na inaendeshwa na Bodi ya Wadhamini inayojulikana kama "Wadhamini Waliosajiliwa wa Uwanja wa Kumbukumbu ya Vita ya Nakivubo", Walioteuliwa na Wizara ya Elimu ya Michezo (Uganda) na Waziri wa Michezo..[5]

Ukarabati Mwaka 2017

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2017, ukarabati mkubwa ulianza kwenye uwanja huo, ikijumuisha uboreshaji wa uwanja, kuongezeka kwa viti kutoka 30,000 hadi 35,000 na ujenzi wa maduka ya rejareja ndani ya kuta za nje za kituo hicho. Ukarabati huo ni ubia kati ya serikali ya Uganda na Ham Enterprises..[9]<ref name=":0">



Viungo ya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. SMC (2013). "Nakivubo Stadium renovations almost complete". London: Stadia-magazine.com (SMC). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-29. Iliwekwa mnamo 7 Julai 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named :0
  3. KAMOGA, JONATHAN. "Ham's shopping grounds create mixed feelings". The Observer - Uganda (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-09. Iliwekwa mnamo 2020-09-02.
  4. FOAC (7 Julai 2017). "Sports in Uganda: Stadia in Uganda". Fortune of Africa.com (FOAC). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-12-01. Iliwekwa mnamo 7 Julai 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 5.2 Reporter (31 March 2015). "M7 Directs Ham Enterprises to Redevelop Nakivubo Staadium". Mukono: Red Pepper. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-23. Iliwekwa mnamo 7 July 2017. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  6. Manishimwe, Wilson (6 Machi 2017). "FDC youth mull court action over leasing of Nakivubo land". New Vision. Kampala. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-23. Iliwekwa mnamo 7 Julai 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Uganda Cranes: From using Inter Milan jerseys to powerful brand - Daily Monitor". monitor.co.ug. Iliwekwa mnamo 23 Juni 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Mukisa, Farahani (30 Machi 2015). "Museveni gives away Nakivubo". Daily Monitor. Kampala. Iliwekwa mnamo 7 Julai 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Ham Enterprises Uganda" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-06-21. Iliwekwa mnamo 19 Juni 2020. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Nakivubo kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.