Wabukusu ni kati ya koo kubwa za Waluhya (Abaluhya) katika magharibi ya Kenya na mashariki-kusini ya Uganda kwenye mitelemko ya mlima Elgon. Eneo lao katika Kenya ni hasa kaunti ya Bungoma. Wako pia Kitale huko Bonde la Ufa.
Idadi yao ilikadiriwa kuwa karibu lakhi sita mwaka 1987.
Wakati wa kuja kwa ukoloni Wabukusu walijaribu kuwazuia Waingereza. Mwaka 1895 walijitetea katika Boma la Chetambe karibu na Bungoma lakini walishindwa na silaha kali za Waingereza.
Upinzani ulirudiwa katika miaka ya 1940 na 1950 Wabukusu wengi walipomfuata Elijah Masinde na jumuiya yake ya Dini ya Musambwa.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wabukusu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |