Wahindi Weusi ni watu wenye asili ya Afrika ambao wanaishi katika nchi za India, Pakistan na Sri Lanka barani Asia. Kwa mwonekano Wahindi Weusi huwa na rangi nyeusi na maumbile ya Kihindi, pia nywele zao ni za singasinga kama walivyo Wahindi asili.
Chimbuko lao ni bara la Afrika kwani ndiyo matokeo ya biashara ya watumwa iliyoshamiri hadi karne ya 19. Watumwa waliochukuliwa Afrika walipelekwa katika maeneo mbalimbali Duniani ikiwemo Amerika lakini wengi zaidi walipelekwa Asia[1] kwa ajili ya shughuli mbalimbali za anasa (hasa wanawake waliofanywa watumwa wa ngono) na uzalishaji mali (hasa wanaume) vkiwemo Kilimo katika mashamba na Uchimbaji wa madini migodini.
Hivyo basi, kadiri siku zilivyokwenda hadi kukomeshwa kwa utumwa kote duniani, watu weusi hao waliendelea kubaki katika maeneo ambayo walikuwa wakifanya kazi na kuingiliana na jamii za wazawa ambako kulipelekea kutokea kwa watoto wenye mchanganyiko wa damu (Chotara) ambao ndio Wahindi Weusi wa leo hii[2].
Wahindi Weusi ni miongoni mwa jamii ambazo zinabaguliwa hadi sasa kutokana na rangi yao nyeusi tofauti na jamii nyingine ya Wahindi kwani wanaamini ni mkosi kuingiliana na watu weusi na kupata nao watoto, hata hivyo watoto waliopatikana wakati wa utumwa walitelekezwa kwa mama zao na kubakia kama jamii inayojitegemea.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wahindi Weusi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |