Western Plains Dogon

Dialekti za magaribi Dogon kwenye ardhi tambarare za magharibi chini ya upande wa Bandiagara Escarpment nchini Mali ni lugha zenye uelewa wa pamoja. Mara nyingine huitwa Kan Dogon kwa sababu hutumia neno 'kan' (pia linaweza kuandikwa kã) kumaanisha aina tofauti za mazungumzo. kama:

  • Tomo kã
  • Teŋu kã
  • Togo kã

Mbili za mwisho mara nyingine hujumuishwa chini ya jina la Tene kã (Tene Kan, Tene Tingi), lakini Hochstetler anazigawanya kwa sababu aina tatu ziko karibu sawa umbali. Kuna takriban wasemaji wa robo milioni wa lugha hizi, kwa kiasi kikubwa wanagawanyika sawa kati ya Tomo Kan na Tene Kan, hivyo kuifanya lugha hii kuwa mojawapo ya lugha zenye idadi kubwa zaidi ya wasemaji kati ya lugha za Dogon. Kuna vijiji vichache vinavyozungumza Tomo karibu na mpaka nchini Burkina Faso."