Zachary Onyonka (1938 - 2002) alikuwa mwanasiasa wa Kenya. Alikuwa mbunge, akiwakilisha Eneo bunge la Kitutu Masaba.
Onyonka alizaliwa mnamo 1938 katika sehemu za Kisii nchini Kenya.
Alichaguliwa mara ya kwanza kama mbunge wa Kitutu West wakati jimbo hili lilipoanzishwa mnamo 1969. Abakia kuwa mbunge wa Jimbo hili la uchaguzi hadi 1988 wakati jimbo hilo liligawanywa na kuzaa jimbo jipya la Kitutu Chache. Onyonka alikuwa mbunge wa jimbo hili jipya hadi kifo chake mnamo 2002.
Onyonka alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje kati ya 1987 - 1988.
Aliaga dunia mnamo 2002 wakati angali akihudumu kama mbunge wa Kitutu Chache.
Alitanguliwa na Elijah Mwangale |
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya 1987-1988 |
Akafuatiwa na Robert Ouko (mara ya pili) |
![]() |
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zachary Onyonka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |