Audie Cornish | |
---|---|
Alizaliwa | 9 Oktoba 1979 |
Nchi | Marekani |
Kazi yake | Mwandishi wa Habari |
Ndoa | Theo Emery |
Watoto | 2 |
Audie N. Cornish[1] (alizaliwa Oktoba 9, 1979) ni mwandishi wa habari kutokea nchini Marekani. Kwa sasa ni muongozaji wa kipindi cha NPR kwa jina la All Things Considered, pia ni mshiriki wa kipindi cha Pop Culture Happy Hour.[2] Hapo kabla alikuwa ni muendesha kipindi cha Profile kilichorushwa na kituo cha BuzzFeed News, kipindi cha mahojiano cha mitandaoni pekee kilichorushwa kwa msimu mmoja tu, pamoja na NPR Presents, kipindi cha mahojiano juu ya kazi, miradi na taratibu mbalimbali zilizolenga kuboresha utamaduni wa Kimarekani.[3]
Cornish alizaliwa jijini Randolph, Massachusetts, wazazi wake ni Wajamaika, na alihitimu elimu yake ya sekondari katika shule ya Randolph High School.[4][5]
Alihitimu elimu ya juu katika chuo kikuu cha Massachusetts-Amherst.[6] Wakati akiwa chuoni, alifanya kazi ya kujitolea katika kituo cha NPR[7][8] na kufanya kazi pia katika kituo cha redio cha chuoni WMUA.
Kazi za hapo awali zilihusisha uandishi wa Habari katika kituo cha NPR la WBUR, shirika la utangazaji na habari la Associated press la jijini Boston, na NPR kuhusiana na masuala ya majimbo kumi ya kusini mwa Marekani pamoja na yale Capitol Hill. Alishirikiana tuzo ya mshindi wa kwanza ya mwaka 2005 katika tuzo ya kitaifa ya uandishi wa kuelimisha (National Awards for Education Writing) juu ya mafanikio ya kitabaka baina ya jamii. Ni mjumbe wa Shirika la waandishi Habari weusi (National Association of Black Journalists).[9]
Kigezo:External media Mnamo Septemba 4, 2011, Cornish alichukua nafasi ya Liane Hansen wa NPR katika kipindi cha Weekend Edition Sunday. Hansen alitayarisha na kuendesha kipind hicho kwa zaidi ya miaka 20.
Mwishoni mwa mwaka 2011, Disemba 18 muendesha kipindi cha Weekend Edition, Cornish aliweka bayana kuwa ataacha kuendesha kipindi hicho na kuhamia katika kipindi cha All Things Considered ifikapo Januari 2012 wakati wa chaguzi za mwaka 2012, kipindi chake kilichukuliwa na mtangazaji mwingine kwa jina la Rachel Martin.[10] Imekuwa ikitajwa sababu ya kuondoka katika kipindi hicho kilisababishwa na mume wake kuwa sehemu ya wanaharakati katika kampeni ya Barack Obama.[11] Mnamo Januari 3, 2013, NPR ilitangaza kuwa Cornish atabakia kuwa muendesha kipindi hicho na Norris atarudi kama muandaaji taarifa wa kipindi.[12]
Mnamo Agosti 2017, Cornish alitangaza kuwa angeondoka NPR wakati atakapopata likizo ya uzazi.[13] Akiwa katika likizo hiyo, alichapisha mahojiano kadhaa katika jarida la The New York Times.[14][15]
All Things Considered ina wasikilizaji takribani milioni 14 kwa wiki.[2][3]
Kuanzia 2018 hadi 2019, Cornish aliendesha kipindi cha televisheni cha kwa jina la Profile kilichohusu taarifa za mbalimbali juu ya mahojiano na kilirushwakupitia mtandao wa Facebook.[16] Kipindi hicho kilidhaminiwa na Facebook, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha uwekezaji wa video katika program ya taarifa za Habari za video kwenye jukwaa lilioandaliwa na mtandao wa Facebook.[17][18] Kila kipande cha Profilekilihusisha mtengeneza taarifa mpya kila wiki, ikiwapa watazamaji nafasi ya kuwasikia watu maarufu kutoka Nyanja mbalimbali kama siasa, teknolojia, biashara na burudani."[18]
Audie Cornish ameolewa na muandishi wa wa kituo cha The Boston Globe Theo Emery.[19] Ana Watoto wawili na mara nyingi amekuwa akiongelea changamoto ya ulinganifu katika kazi na familia.[20]
{{cite news}}
: More than one of |accessdate=
na |access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Cornish, originally from Boston and a 2001 graduate of the University of Massachusetts-Amherst with a bachelor's degree in journalism...
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite news}}
: More than one of |accessdate=
na |access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: More than one of |accessdate=
na |access-date=
specified (help)
{{cite news}}
: More than one of |accessdate=
na |access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Audie Cornish kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |