Clément Cailleau

Clément Cailleau C.S.Sp. (27 Julai 192321 Julai 2011) alikuwa kasisi na kiongozi wa Kanisa Katoliki aliyezaliwa Ufaransa. Alihudumu kama prefekti wa eneo ambalo sasa ni Jimbo Katoliki la Tambacounda, Senegal, kuanzia tarehe 13 Agosti 1970 hadi 24 Aprili 1986. Tambacounda lilipandishwa hadhi kuwa jimbo kamili la Kanisa Katoliki mwaka 1989.

Cailleau alizaliwa Nueil-sur-Layon, Ufaransa, tarehe 27 Julai 1923. Alipadrishwa kuwa kasisi wa Shirika la Roho Mtakatifu (Holy Ghost Fathers) tarehe 1 Oktoba 1950.

Alifariki tarehe 21 Julai 2011 akiwa na umri wa miaka 87, kama prefekti mstaafu wa Tambacounda.[1]

  1. "Father Clément Cailleau, C.S.Sp. †". Catholic Hierarchy. Iliwekwa mnamo 2011-07-28.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.