Cyril Lincoln Sibusiso Nyembezi (6 Desemba 1919 - 25 Juni 2000) alikuwa mwandishi, mwalimu na mhariri wa Afrika Kusini. Hasa aliandika kwa lugha yake ya Kizulu.
Nyembezi alizaliwa tarehe 6 Desemba 1919 eneo la Babanango nchini Afrika Kusini. Babake alikuwa mchungaji wa kanisa la Methodist. Alisomea Chuo Kikuu cha Witwatersrand mjini Johannesburg akapata shahada ya kwanza mwaka wa 1947 na ya pili mwaka wa 1954. Alimwoa Muriel mwaka wa 1950 wakawa na watoto wanne. Baada ya kufundisha lugha ya Kizulu katika vyuo vikuu vya Johannesburg na Fort Hare, akawa mhariri wa kampuni la Shuter na Shooter mjini Pietermaritzburg kuanzia mwaka wa 1959.
![]() |
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Cyril Nyembezi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |