Daraja la Rusumo English: Rusumo Bridge | |
---|---|
![]() | |
Yabeba | Barabara kuu ya B3 (leni 1) |
Yavuka | Mto Kagera |
Urefu | mita 100 |
Upana | mita 3.5 |
Kiasi cha mzigo | tani 8 |
Yafuatiwa na | Daraja la Kyaka |
Anwani ya kijiografia | 2°22′56.35″S 30°46′59.64″E / 2.3823194°S 30.7832333°E |
Mahali ya daraja nchini Tanzania |
Daraja la Rusumo ni daraja la kimataifa linalovuka Mto Kagera na kuunganisha nchi jirani za Rwanda na Tanzania.
Daraja la kwanza ni feleji lenye urefu wa mita 64 lililotengenezwa huko Torino nchini Italia kuanzia mwaka 1966, kusafirishwa hadi Tanzania na kuunganishwa mahali pake mwaka 1972.
Tarehe 28 Aprili 1994, wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, zaidi ya wakimbizi 200,000 walipitia daraja hilo katika muda wa masaa 24. [1]
Kutokana na kuongezeka kwa usafiri wa kupitia daraja hilo, halikutosha tena, hasa kwa sababu ni jembamba: kuna njia moja pekee kwa magari. Vilevile lilikadiriwa kubeba tani 56 ambazo ni uzito unaopitiwa na malori makubwa. Hivyo mpango wa kujenga daraja jipya ulianzishwa mwaka 2012.
Daraja la pili la Rusumo lilikamilishwa kando ya daraja la kale kwenye mwaka 2014. Daraja hilo lilijengwa na kampuni ya Japani ya Daiho Corporation Company[2]. Daraja lilitengenezwa vipandevipande huko Japani, kupelekwa Dar es Salaam na kusafirishwa hadi Rusumo ambako vipande viliunganishwa.
Daraja jipya huwa na njia mbili za magari likiwa na uwezo wa kubeba tani 400 kwa wakati mmoja.[3]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)