Edward Sokoine

Edward Moringe Sokoine

Edward Moringe Sokoine (1 Agosti 1938[1] - 12 Aprili 1984) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Tanzania.

Aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili, tangu tarehe 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980, tena tangu tarehe 24 Februari 1983 hadi kifo chake, alipofariki kufuatana na ajali ya gari.

Uongozi wake ulionekana kuwa wa mfano kwa jinsi alivyokuwa na uadilifu na kufuatilia utendaji kazi huku akikemea ulaji rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.

Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki, tena mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.

Kwenye mwaka 1984 jina la Sokoine lilitajwa mara kadhaa katika majadiliano kuhusu rais mpya baada ya Nyerere yaliyoanza wakati ule[2]. Lakini alifariki kwa ajali ya gari wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam. Kifo hiki kilisababisha masimulizi mbalimbali yenye wasiwasi kuhusu ajali hii kuwa ilipangwa[3].

Kifo chake kilileta majonzi makubwa kwa Watanzania wa kawaida ambao walikuwa wanamtarajia kuwatetea wanyonge na kuinua hali ya maisha yao.

Mwili wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli, mkoani Arusha[4].

Sokoinie anakumbukwa hadi leo (2019)[5]. Chuo cha Kilimo na Mifugo Morogoro kilipewa jina la "Chuo cha Kilimo cha Sokoine" ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Sokoine.

  1. Edward Moringe Sokoine - B. S. Swebe - Google Books. Iliwekwa mnamo 2012-01-10 – kutoka Google Books.
  2. Reuters. "TANZANIAN PREMIER IS KILLED; WAS LEADER'S HEIR APPARENT", 1984-04-13. 
  3. Foul play tales on Sokoine’s death, The Citizen Tuesday April 12 2016, iliangaliwa Aprili 2019
  4. "SPECIAL REPORT: The life and times of Edward Sokoine: man of action". 
  5. PM tasks authorities to improve memorial site in memory Sokoine, ipp-media vom 12.04. 2019

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edward Sokoine kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.