Henry Wanyoike (alizaliwa 1974) ni Mwanariadha wa Kenya aliye Kipofu. Anashiriki katika mashindano ya Paralympics katika shindano la Marathon.
Wanyoike ni mmoja wa Wanariadha wa kasi sana duniani. Alianza kukimbia akiwa mtoto na tayari alikuwa na ndoto ya kujiunga na kundi la Kenya la wanariadha, nchi ambayo inajulikana kwa kuwakuza Wanariadha wengi wa Massafa marefu wa Kimataifa kuliko nchi nyingine yoyote.
Alitia fora katika mita 5000 na mita 10,000.
Mnamo 1995, Wanyoike alikuwa kipofu wakati alipata mshtuko. Alisimulia, "Nilienda kitandani nikiwa mzima, kuamka nikaamka kwa giza". Usiku huo alipoteza karibu asilimia 95 ya uwezo wake wa kuona na polepole akiupoteza wote. "Nilifikiria maisha yangu yamefikia kikomo",[1] anasimulia.
Mamaye Grace alimchukua katika kliniki ya macho ya Kikuyu[2], (Hospitali ya karibu ya macho inayodhminiwa na shirika la [[Christian Blind Mission International]], CBMI), inayotambulika kama moja ya vituo bora zaidi vya watu walio na shida ya macho katika eneo la Afrika Mashariki.
Petra Verweyen, msimamizi wa mradi wa Low Vision alimsaidia kujipanga tena kimaisha na akampanga kujifunza kushona fulana. Kwa shukrani kubwa alikubali mradi huo na kuahidi kuwasaidia vipofu wengine kujitegemea kimaisha , vile amefanya.
Baada ya kushinda Nishani ya Dhahabu kule Sydney, Australia katika Mashindano ya Paralympic ya 2000, Wanyoike amenunua mashine nyingi za kushona kutokana na zawadi ya fedha alizokabidhiwa na watu maarufu kama vile Arnold Schwarzenegger. Saa hii yeye ni mwajili wa watu wengine vipofu wa Kenya na kuwafunza kufuma fulana.
Mwanariadha kopofu huwa na mtu wa kumwongoza aliyefunganishwa naye mkononi. Kiongozi hutumia kiunganishi hiki kumwashiria mwanariadha, bila kumzidi kasi, wakati wa kugeuka, kupunguza kasi na kuhepa kizuizi, iwe kiwanjani au barabarani. Henry alipozoea kushirikiana na viongoza, alichipuka haraka kama mwanariadha kipofu wa kimataifa.
Hili lilimpatia nafasi katika kikundi cha Kenya cha kuwakilisha Kenya katika mashindano ya Sydney ya Paralympics ya 2000 katika shindano la mita 5000.
Tatizo lililoibuka ni kuwa viongozi wake hawangestahimili kasi yake. Hata hivyo, licha ya kushinda medali ya Dhahabu katika mashindano ya Paralympics, aliweka pia rekodi mpya ya Paralympics. Sasa hivi Wanyoike hukimbia na Kiongozi wake na rafiki taangu utoto, Joseph Kibunja.
Kinyume na washindani wengi ambao huboresha ujuzi wao katika shindano moja, Henry ni mmoja wa wale ambao wamejiboresha katika mashindano mengi. Katika miaka 10 iliyopita, ameshiriki katika mashindano ya Half-Marathon, mbio za barabarani za kilomita 10, mita 5,000 na mita 1,500. Anashikilia rekodi ya Dunia ya Marathon kwa vipofu ya 2:31:31 aliyoiweka jijini Hamburg mnamo 2005.
half-marathon (1:14:44) - washiriki 2,675
half-marathon (1:16:47) - Washiriki 9000
(2:52) - washiriki 177 pekee kati 3000 walimaliza kwa wakati (saa 5)
half-marathon (1:16:07)
mjini Palma, Mallorca (1:15:24)
mjini Wetzlar (01:14:41)
katika mashindano ya half-marathon ya Hannover (1:11:25)
Hamburg: 2:31:31
London: 2:32:51
ya Dunia katika mashindano ya 5,000 m (15:11.07) na 10,000 m (31:37.25) jijini Athens
ya shindano lahalf marathon (1:10:26)
katika umbali wa zaidi ya mita 1500
na 10,000
(2:49:03)
rekodi ya Dunia ya mita 5,000 (15:17.75) na mita 10,000 (32:34.31)
vipofu ya marathon ya Japan
katika mashindano ya mita 800 na 1500, Fedha katika shindano la mita 400
5,000 (15:46.29)