Immaculate Chemutai

Immaculate Chemutai (alizaliwa 2 Desemba 1987) ni mwanariadha wa Uganda wa mbio za marathoni. [1]

Mnamo tarehe 9 Februari 2020, Chemutai aliweka rekodi mpya ya kitaifa kwa mbio za marathon za wanawake za Uganda kwa kutumia saa 2:32:41 katika mbio za Buriram Marathoni.[2]

Chemutai alitumia saa 2:29:09 wakati wa Mbio za Xiamen mnamo Aprili 11 2021, ili kuweka ubora mpya wa binafsi na kufikia kiwango cha kufuzu kwa Olimpiki. Alithibitishwa kama mshiriki wa timu ya Olimpiki ya Uganda kwa Olimpiki ya Tokyo mwaka 2020 iliyocheleweshwa, Mei 2021.[3]

Alishiriki katika mbio za marathoni za wanawake katika Mashindano ya Riadha ya Dunia mwaka 2022 yaliyofanyika Eugene, Oregon, Marekani.

  1. "Immaculate CHEMUTAI | Profile". worldathletics.org.
  2. "Marathon Prize Winners". Race REsult. 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-24. Iliwekwa mnamo 2022-08-09.
  3. "Kiprotich finally selected for Tokyo olympics". The Independent (Uganda). 4 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 18 Juni 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Immaculate Chemutai kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.