Jane Fernandes

Jane Fernandes katika sherehe za mahafali ya kutunuku shahada wanafunzi huko North Carolina.

Jane Fernandes (alizaliwa 21 Agosti 1956) ni mwalimu na mtetezi wa haki za kijamii wa Marekani.

Kuanzia Agosti 2021, Fernandes alikuwa Rais wa Chuo cha Antiokia huko Yellow Springs, Ohio.[1] Hapo awali aliwahi kuwa rais wa Chuo cha Guilford kutoka 2014 hadi 2021.

Mwaka 1990, Fernandes alikuwa mwanamke wa kwanza kiziwi kuongoza shule ya Marekani iliyoanzishwa kwa ajili ya viziwi, wasioona, na viziwi wasioona, aliwahudumia huko Honolulu Marekani hadi Agosti 1995.

  1. YS News Staff (2021-08-04). "Antioch College names new president". The Yellow Springs News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-07-21.