Jeshi la Ardhi la Kenya ni tawi la wanajeshi wa ardhini la Majeshi ya Ulinzi ya Kenya.
Jeshi la leo lilitokana na King's African Rifles.[1]
Mwezi Agosti 1895, serikali ya Uingereza ilikubali kuanzishwa kwa kikosi kilichojumuisha Wapunjabi 300, Waswahili 300, Wasudani 100 na wanajeshi 200 kutoka makabila mbalimbali katika kanda. Kikosi hicho kiliitwa East African Rifles na kilikuwa kimetengenezwa kutoka kikosi cha awali, IBEA katika Mombasa (Fort Jesus).
King's African Rifles walipigana dhidi ya Mau Mau chini ya amri ya maafisa wa Uingereza na upande Wakenya waaminifu kwa wakoloni na wale ambao walitetea amani ili kupata uhuru, kama vile Jomo Kenyatta.
Mbali na jukumu la msingi la ulinzi wa Jamhuri ya Kenya na jukumu la misaada kwa mashirika ya mamlaka, Jeshi la Kenya hushiriki katika shughuli za kudumisha amani ya kimataifa. Jeshi la Kenya lilijihusisha na shughuli za misaada ya amani mwaka 1973 lilipokubali ombi la Umoja wa Mataifa kwa Jamuhuri ya Kenya kutoa vikosi baada ya vita vya Waarabu na Waisraeli. Hata hivyo, jeshi halikuweza kujifikisha kwa sababu ya matatizo katika uhamishaji.
Mara ya kwanza ya Jeshi la Kenya kushiriki kikamilifu katika kudumisha amani ilikuwa mwaka 1979, wakati Jumuiya ya Madola iliomba Jamhuri ya Kenya kuchangia wanajeshi ili kudumisha amani katika Rhodesia ya Kusini (sasa Zimbabwe). Nchi ilikuwa inakabiliwa na vita vya ukombozi.
Tangu mwaka 1989, Kenya imechangia waangalizi wa kijeshi, wafanyakazi, polisi wasimamizi wa raia na wanajeshi wa miguu.[2] Kiwango cha ushiriki huo umejumuisha makamanda wa vikosi, mwangalizi mkuu wa jeshi, Majenerali wakuu katika misheni zifuatazo za UM na UA:
Kwa sasa, walinzi amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Kenya wametumika katika nchi 16 tofauti katika Afrika, Mashariki ya Kati, Balkani na Asia.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)