Joakim Segedi

Joakim Segedi (27 Oktoba 190420 Machi 2004) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Kiruteni kutoka kwa watu wa Ruthenia na Kroatia.

Alikuwa askofu msaidizi wa Eparkia ya Križevci ya Kanisa hilo la Mashariki kama askofu wa jimbojina la Gypsaria kutoka mwaka 1963 hadi 1984.

Tarehe 17 Machi 2004, siku tatu kabla ya kifo chake, alipewa hadhi ya kuwa askofu mkuu.[1]

Alizaliwa katika Ruski Krstur, Austria-Hungaria (ambayo sasa ni sehemu ya Serbia) mwaka 1904, alifanywa kuwa padri tarehe 4 Septemba 1927 na Askofu Dionisije Njaradi kwa ajili ya Jimbo la Križevci. Padre Segedi alikuwa mkurugenzi wa kiroho wa Seminari ya Kanisa Katoliki la Kigiriki huko Zagreb kutoka mwaka 1930 hadi 1936 na msaidizi binafsi wa Askofu kutoka mwaka 1936 hadi 1940.

Aliteuliwa na Papa Yohane XXIII kuwa Askofu Msaidizi tarehe 24 Februari 1963. Aliwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 28 Julai 1963. Mwekaji wakfu mkuu alikuwa Metropolitan Yosyf Slipyi, na washiriki wa msaidizi katika uwekaji wakfu walikuwa Askofu Mkuu Gabrijel Bukatko na Askofu Augustine Hornyak huko Roma.

Askofu Segedi alistaafu kama Askofu Msaidizi tarehe 27 Oktoba 1984 akiwa na umri wa miaka 80.

Alishiriki katika Mtaguso wa pili wa Vatikani katika miaka ya 1960. Alifariki dunia huko Križevci tarehe 20 Machi 2004.[2]

  1. "Archbishop Joakim Segedi". catholic-hierarchy.org. 2016-06-07.
  2. Blazejowsky, Dmytro (1988). Ukrainian Catholic clergy in diaspora (1751-1988). Rome. uk. 204.{{cite book}}: CS1 maint: location missing publisher (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.