Job Yustino Ndugai (amezaliwa 21 Januari 1960) ni mbunge wa jimbo la Kongwa katika bunge la kitaifa nchini Tanzania.[1] Anatokea katika chama cha CCM.
Tangu tarehe 17 Novemba 2015 hadi 6 Januari 2022 alikuwa Spika wa Bunge la Tanzania. Baada ya kuingia katika ugomvi na rais Samia Suluhu Hassan alipaswa kujiuzulu uspika[2].
![]() |
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |