Joseph Albert Rosario, M.S.F.S (30 Mei 1915 – 31 Julai 2011) alikuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka India. Alikuwa mmoja wa maaskofu wa Kanisa Katoliki wa muda mrefu zaidi na ndiye aliyekuwa askofu mzee zaidi kutoka India.
Rosario alizaliwa mjini Nagpur, India, tarehe 30 Mei 1915. Alipadrishwa kuwa kasisi tarehe 29 Septemba 1944 katika shirika la Wamisionari wa Mt. Francis de Sales.
Mnamo tarehe 8 Mei 1955, aliteuliwa kuwa askofu wa Jimbo la Amravati, na akapewa daraja ya uaskofu tarehe 13 Novemba 1955.
Alistaafu kutoka uongozi wa jimbo hilo tarehe 1 Aprili 1995.[1]
http://www.catholic-hierarchy.org/bishop/brosar.html
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |