Amezaliwa | 2 Januari 1968 Dar es Salaam |
---|---|
Nchi | Tanzania |
Kazi yake | Mtaalamu wa mazingira |
Joyce Msuya (alizaliwa Dar es Salaam, 2 Januari 1968) ni mwanabiolojia na mtaalamu wa mazingira kutoka Tanzania, aliyekuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa UM kwa Shughuli ya Hisani na mratibu msaidizi wa miradi ya misaada ya hisani ya Umoja wa Mataifa.[1].
Hadi kuteuliwa kwa kazi hiyo Desemba 2021 alikuwa Kaimu Mkurugenzi Tekelezi wa Mradi wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mazingira (UNEP) na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UM tangu mwaka 2018.[2].
Joyce Msuya ni mtoto wa nne wa Cleopa Msuya aliyekuwa Katibu wa Wizara ya Uchumi na Mipango akaendelea kuhudumia kama Waziri Mkuu wa Tanzania mara tatu.
Alianza masomo kwenye shule ya msingi ya Forodhani, Dar es Salaam akamaliza Form VI Shule ya Sekondari ya Weruweru kwenye mkoa wa Kilimanjaro[3].
Alisoma Chuo Kikuu cha Strathclyde, Glasgow (Uskoti) alipopokea mwaka 1992 shahada ya kwanza katika somo la biokemia. Akaendelea na masomo yake Chuo Kikuu cha Ottawa, Kanada alipohitimu mwaka 1996 kwa shahada ya uzamili ya mikrobiolojia na elimu ya kingamaradhi[4].
Ameolewa na Onesmo Mpanju akazaa watoto wawili.
Baada ya kumaliza masomo Msuya alikuwa na ajira za muda mfupi hadi kuajiriwa na Benki ya Dunia kwenye mwaka 1998[5] alipoendelea hadi mwaka 2018 katika nafasi mbalimbali, pamoja na kuwa mwakilishi wa benki katika Jamhuri ya Korea.
Kwenye Agosti 2018 alihamia ofisi kuu ya Umoja wa Mataifa akipewa nafasi ya Naibu Mkurugenzi Tekelezi wa UNEP. Baada ya kujiuzulu kwa Mkurugenzi Tekelezi Erik Solheim[6] kwenye Novemba 2018 amekuwa kaimu mkurugenzi tekelezi.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Joyce Msuya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |